Na Amiri Kilagalila, Njombe
JESHI la Polisi mkoani Njombe linawashikilia walimu wawili wa shule ya sekondari Mang’oto wilayani Makete mkoani Njombe kwa tuhuma za kumsababishia ujauzito na kumtoa mwanafunzi wa shule hiyo mwenye umri wa miaka 17.
Akizungumza na vyombo vya habari, kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Njombe, Hamis Issa amesema wanamshikilia mwalimu Ezekiel Thomas (36) maarufu kwa jina la Dokole kwa kuwa na mahusiano na mwananfunzi na kumsababishia ujauzito.
“Huyu mwalimu amekuwa na mahusiano na mtoto wa sekondari mwenye umri wa miaka 17 na binti huyo amepimwa amegundulika ni mjamzito.” Alisema kamanda Issa
Aidha amesema wanamshikilia mwalimu, Ben Liamdilo (35) kwa kushirikiana katika tukio la utoaji wa mimba na kumsababishia maumivu mwanafunzi huyo.
“Mwalimu Thomas alifanya juhudi akamtuma huyu mwalimu mwenzake akambeba na boda boda kwenda kumtoa mimba mpaka sasa hivi walimu wote wawili tunawashikilia na wanatuhumiwa na makosa haya.”Alisema kamanda Issa
Vile vile ameitaka jamii kushirikiana kwa kutoa taarifa kwa jeshi la Polisi ili kukabiliana na vitendo kama hivyo.
Kamanda wa jeshi la Polisi mkoa wa Njombe, Hamis Issa akizungumza na waandishi wa habari.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment