WAZIRI AWESO ATANGAZA VITA KWA EWURA KWA KUSHINDWA KUSIMAMIA MAJUKUMU YAO | Tarimo Blog

WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso ametangaza vita kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na maji (EWURA) kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo katika udhibiti wa maji.

Aweso ameyasema hayo wakati akifunga kikao kazi cha wizara ya maji na taasisi zake iliyobeba kauli mbiu ya mageuzi ya sekta ya maji.

Alisema EWURA haifanyi vizurii katika udhibiti wa maji wananchi wanabambikiziwa bili bila sababu ya msingi na wao kama wadhibiti wametulia tu.

"Jumatatu nakuja huko ntawakalia kooni kwasababu malalamiko yamekuwa mengi na ninyi kama mamlaka inayohusika na hayo malalamiko mmetulia, nataka nikija mnieleze kwani ni wananchi wanabambikiziwa bili mnawasababishia wananchi wanaona kama wizara haifanyi kazi" alisema

Aweso aliwataka wakurugenzi wa mamlaka za maji mkoa na wilaya kuhakikisha wanasimamia miradi ya maji ili kuhakikisha maji yanakuwa ya uhakika kwenye maeneo yao kwani hakuna mbadala wa maji.

Aweso pia amewataka wadhibiti ubora wa maji kuhakikisha maji yanayopatikana yanakuwa safi na salama kwa matumizi ya binadamu lengo ni kuona wananchi wanaridhika na huduma inayotolewa na sekta hiyo.

"Wakurugenzi msikae ofisi hakikisheni mnatembea miradi ya kuzalisha maji katika maeneo yenu angalau kwa wiki Mara tatu hiyo itasaidia kugundua matatizo ya miradi mapema kabla haijafikia kwenye hatua ya kuleta itilafu wananchi wakakosa maji" alieleza

Kwa upande wake naibu waziri wa maji Maryprisca Mahundi aliwataka wakurugenzi kuhakikisha miradi inayotekelezwa inakamilika kwa wakati kwa kutumia wataalamu wa ndani ilikupunguza gharam.

Alisema amefanya ziara katika baadhi ya mikoa na wilaya alikuta miradi inasua sua alichukua hatua kwa baadhi ya wakurugenzi wengine walipewa onyo lengo sio kugishiana bali ni kuhakikisha kazi tuliyopewa na wananchi tunaitekeleza kwa wakati.

"Mimi ntazidi kuwa mkali kwa wakutugenzi ambapo wanawafuga wahandisi wanaochelewesha miradi ya wananchi nataka kuona kila mahala palipo na miradi inatekelezwa kwa wakati kwasababu serikali inatoa fedha hivyo hatuna haja ya kuvhelewesha miradi" alisema

Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba alisema mipango ya serikali ni kuhakikisha kila mwananchi anapata maji safi na salaama bila kujali anaishi wapii.

Alisema huduma ya maji safi na salama kwa uhakikika haitaishia mijini tu Bali hata vijijini wananchi wanahaki ya kupata maji safi na salama, fedha zote zinazotolewa na serikali ni kuhakikisha jambo hill linafanyika kwa vitendo

" Serikali inamipango mathubuti kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma ya maji safi na salaama kwani maji ni sekta muhimu katika jamii na hakuna mbadala wa maji kama zilivyo nguo,chakula na vinywaji" Amesema.




 
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2