WAZIRI UMMY AKUMBUSHA MALEZI BORA KWA WATOTO, AAHIDI KUWA MWANAJUMUIYA IDARA YA WANAWAKE MASJID AKRAM | Tarimo Blog

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Ummy Mwalimu akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu waliofika katika Msikiti wa Akram, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam kuadhimisha Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhamad (s.a.w). Maulid hiyo ilifanyika Januari 9, 2021.
Makamu Mwenyekiti wa Idara ya Wanawake Masjid Akram, Zainab Asman Kasoro akizungumza jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Ummy Mwalimu wakati wa Maulid ya Mtume Muhamad (S.A.W), Maulid iliyofanyika Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Wasichana kutoka Madrasa wakiimba Qaswida za kutukuza 
Mtume Muhamad (S.A.W) katika Maulid ya kuadhimisha mazazi yake.

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhe. Ummy Mwalimu amekumbusha malezi bora kwa Wazazi wenye watoto hasa Watoto wa Kike. 

Waziri Ummy ameyasema hayo katika Maulid ya Kuzaliwa Mtume Muhamad (S.A.W). Maulid hiyo iliyofanyika Januari 9, 2021 katika Msikiti wa Akram uliopo Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.

“Ndugu zangu Waislamu katika kushereherekea Maulid hii, tukumbuke kushikamana lakini nawahusia kutimiza wajibu wenu katika malezi, makuzi na matunzo kwa Watoto, tumeikamata dunia tumejisahau kutoa malezi bora.” amesema Waziri Ummy.

“Nilikuwa Waziri wa masuala ya Maendeleo ya Wanawake na Watoto, kwa kweli Watoto wa Kike, Kiume wana lawitiwa sana unajiuliza hivi Mtoto ana wazazi Nyumbani na analawitiwa mwezi mzima, unajiuliza Wazazi wako wapi.” Aliuliza.

Waziri Ummy amehasa wazazi kuhakikisha wanatoa malezi bora kwa Watoto hao, pia kuhimiza Elimu Dunia na Akhera.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Idara ya Wanawake, Masjid Akram, Mwajuma Kingwande amesema wameadhimisha Maulid hiyo ya Mtume Muhamad (S.A.W) ili kuhamasisha Kizazi cha sasa na kijacho kuona umuhimu wa siku hiyo na kufuata Sifa zake, tabia, mwenendo wake kizazi cha sasa.

Amesema Idara ya Wanawake Masjid Akram inajihusisha pia na masuala ya kijamii kama kufutirisha kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan kwa wasio na uwezo pia kutembelea vituo vya Watoto yatima sambamba kutoa misaada ya kijamii bila kujali dini.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2