Ofisi ya Jumuiya ya watumia maji kijiji cha Likuyusekamaganga ambayo itatumika kwa ajili ya uendeshaji wa mradi wa maji wa Likuyusekamaganga utakaowanufaisha wananchi wa kijiji hicho na kijiji cha Mandela wilayani Namtumbo mradi uliotekelezwa na wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa,
****************************************
Na Muhidin Amri,Namtumbo
WAKALA wa maji na usafi wa mazingira (Ruwasa) katika wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma, umeokoa kiasi cha shilingi milioni 560,000.000 kati ya shilingi bilioni 4,915,864.910 zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji wa Likuyusekamaganga wilayani humo.
Kuokolewa kwa kiasi hicho cha fedha, kumetokana na uamuzi wa wizara ya maji kujenga mradi huo kwa kuwatumia mafundi wadogo chini ya usimamizi wa wakala wa maji na usafi wa mazingira(Ruwasa) kwa mfumo wa force akaunti ambapo gharama za ujenzi zimepungua hadi kufikia shilingi bilioni 3,578,363.191.
Awali mradi wa maji Likuyusekamaganga ulisainiwa na kuanza kujengwa mwaka 2017 na ulitakiwa kukamilika mwaka 2020 na mkandarasi kampuni ya Elgance Developers Co Ltd kwa gharama ya shilingi bilioni 4,915,864.910.
Hata hivyo, wizara ya maji ilivunja mkataba mwishoni mwa mwaka uliopita kufuatia mkandarasi kushindwa kukamilisha kwa muda uliopangwa na kukabidhi mradi huo kwa Ruwasa kwa ajili ya utekelezaji wake.
Meneja wa Ruwasa wilaya ya Namtumbo Mhandisi David Mkondya alisema, kupungua kwa gharama za wa mradi ni baada ya Ruwasa kuanza kujenga kwa kwa utaratibu huo ambapo umekamilika kwa asilimia 90 na hadi sasa fedha zilizotumika ni bilioni 2,745,992.944.
Alisema, mradi unalenga kutawanufaisha zaidi ya wakazi 13,320 kutoka vijiji viwili vya Likuyusekamaganga na Mandela.
Alisema tangu Ruwasa ikabidhiwe mradi, kazi zilizofanyika ni ujenzi wa chanzo,nyumba ya mlinzi,ofisi ya jumuiya ya watumia maji,ujenzi wa bomba kuu kutoka chanzo hadi kwenye matenki, na ujenzi wa bomba la usambazaji ambao bado unaendelea.
Alitaja kazi nyingine zilizokamilika ni ujenzi wa matenki mawili,vituo 53 vya kuchotea maji,pampu ya kuvuta maji na mfumo wa umeme jua umenunuliwa na kufungwa.
Aidha, alisema kazi ambazo bado zinaendelea ni kumalizia ujenzi wa ofisi ya jumuiya ya watumia maji,kumalizia jengo la muhudumu wa pampu,uunganishaji wa mtambo wa usambazaji maji katika vijiji husika.
Alisema, changamoto kubwa katika Utekelezaji wa mradi huo mzabuni kuchelewa kuleta bomba za kukamilisha mradi kwa awamu,lakini Ruwasa inaendelea kufuatilia kwa mzabuni kuleta bomba zilizobaki.
Kwa upande wao baadhi ya wakazi wa kijiji cha Likuyusekamaganga, wameelezea furaha yao kwa Serikali ya awamu ya tano kwa kujenga mradi huo wa maji ambao unakwenda kumaliza changamoto ya muda mrefu ya huduma ya maji.
Abdala Haule alisema, amefurahishwa na mkazo mkubwa uliowekwa katika ujenzi wa mradi huo hasa kutokana na ukweli kwamba mradi ulianza kujengwa zaidi ya miaka mitano iliyopita na bado haujakamilika.
Sihaba Baigwa alisema, msukumo uliofanywa na Ruwasa katika kukamilisha ujenzi wa mradi wa maji Likuyusekamaganga ni ishara kwamba Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kumaliza kero zilizokuwepo kwa muda mrefu kwa kuboresha huduma za kijamii na maisha ya wanancMafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment