TAYARI KATIBU MKUU BAKWATA TAIFA AMEWASILI MKOANI KAGERA. | Tarimo Blog

Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mwl. Jabir Nuhu Mruma amewasili  Mkoani Kagera kwa Ziara ya Kikazi ikiwa no Sambamba na Kuhudhuria Maulid na Harambee iliyoandaliwa na BAKWATA Kagera kwa Kushirikiana na Akina Mama wa Kiislamu wa Kamachumu.

Akina Mama hao wa Kikundi cha Fiisabilillah wameandaa Maulidi na Harambee hiyo maalumu kwa ajili ya Kuchangia Ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kamachumu Islamic English Medium Primary iliyopo Kamachumu. Tukio Hilo linafanyika kesho Jumamosi katika Viwanja vya Shule hiyo Ambapo watu wote Dini zote wamealikwa kuunga Mkono juhudi hizo.  Katibu Mkuu BAKWATA kapokelewa Uwanja wa Ndege na Viongozi mbalimbali wa Dini wakiongozwa na Sheikh Mkuu wa mMkoa Kagera Alhaji Kichwabuta





 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2