WAANDISHI WA HABARI WAASWA KUENDELEA KUANDIKA NA KUSAMBAZA HABARI ZA MAENDELEO NDANI NA NJE YA NCHI | Tarimo Blog

WAANDISHI wa habari za Uchumi Biashara na Fedha wametakiwa kuendelea kuandika na kusambaza habari kuhusu jitihada mbalimbali za maendeleo zinazofanywa na Serikali ndani na nje ya mipaka ya Nchi.

Akisoma hotuba wakati wa kufunga mafunzo ya siku tano kwa waandishi wa habari za Uchumi, Biashara na Fedha Meneja Uendeshaji BoT Tawi la Mtwara Graceana Bemeye kwa niaba ya Mkurugenzi wa tawi la Benki Kuu ya Tanzania (BoT,) tawi la Mtwara Bw. Lucas Mwimo,amesema, mafunzo hayo ambayo yamekuwa yakitolewa kwa miaka saba mfululizo ni kutokana na umuhimu wa vyombo vya habari katika kuhabarisha Umma wa watanzania kuhusiana na maendeleo mbalimbali yanayotekelezwa nchini.

"Tumeshuhudia habari zenu nyingi zikirushwa, kutangazwa na kuandika katika vyombo vya habari kuhusu kila kilichojiri katika semina hii kwa kipindi chote mlichokuwa hapa Mtwara, tuimarishe nguzo hii kwa kuhakikisha jamii inapata habari za kujenga na kuelimisha zaidi." Amesema.

Aidha amewashauri wanahabari hao kupeleka maarifa waliyoyapata katika mafunzo hayo kwa jamii.

"Semina hizi zitaendelea kuandaliwa mara kwa mara kwa kuthamini mchango wenu na katika kumuenzi marehemu Prof. Benno Ndulu Gavana wa benki Kuu aliyeasisi uendeshaji na mafunzo haya, kwa kuamini yatawajengea uwezo wa kuelimisha na kufafanua masuala mbalimbali yanayohussu majukumu na kazi za Benki Kuu na ninaamini kupitia ninyi jamii imepata kujifunza na itajifunza mengi zaidi kuhusiana na majukumu ya Benki Kuu pamoja na mada nyingine nyingi ambazo zimetolewa katika mafunzo haya." Amesema.

Ameeleza, kama alivyoeleza Naibu Gavana wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, Benki Kuu itaendelea kudumisha mahusiano mema na vyombo vya habari ambavyo vimekuwa vikichangia katika maendeleo ya taifa kwa namna mbalimbali ikiwemo kuhabarisha,kutoa taarifa za miradi mbalimbali ya kiuchumi pamoja na kuibua fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo na ambazo zikitumika vizuri zinaweza kuchangia ukuaji wa uchumi na kuongeza pato la taifa.

Katika Semina hiyo mada mbalimbali ikiwemo majukumu ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT,) misamiati na dhana mbalimbali zinazotumika katika habari na taarifa za kifedha na uchumi pamoja na uchambuzi wa ripoti za fedha zilitolewa huku Ofisini ya Makosa ya Jinai na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji Tanzania (CMSA)wakitoa mada kuhusu upatu haramu.

Meneja Uendeshaji Tawi la BoT Mtwara Bi.Graceana Bemeye akisoma hotuba ya kufunga mafunzo ya siku tano kwa waandishi wa habari za Uchumi, Biashara na Fedha kwa niaba ya Mkurugenzi wa Tawi la BoT Mtwara yaliyofanyika BoT tawi la Mtwara.

Pichani kulia ni Meneja Msaidizi wa Idara ya Uhusiano wa BoT, Vicky Msina akimtambulisha Mkurugenzi wa Usimamizi wa Sekta ya Fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT),Bwa.Jery Sabi kwa Waandishi wa habari za Uchumi, Biashara na Fedha
Mkurugenzi wa Usimamizi wa Sekta ya Fedha kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT),Bwa.Jery Sabi akieleza kwa kifupi mbele ya waandishi wa habari za Uchumi, Biashara na Fedha kuhusu mafunzo yanayotolewa kwa maafisa Maendeleo ya Jamii nchini kuhusu kuanza kutumika kwa mfumo maalumu wa kusajili vikundi vya VICOBA nchini,ambapo amesema mafunzo hayo yatafanyika katika Kanda tano na kukoma Machi 15,2021.
Meneja Msaidizi Idara ya Uhusiano wa BoT, Vicky Msina akimkaribisha Meneja Uendeshaji Tawi la BoT Mtwara Bi.Graceana Bemeye (pichani kushoto) kufunga mafunzo ya siku tano ya Waandishi wa habari za Uchumi, Biashara na Fedha kwa niaba ya Mkurugenzi wa Tawi la BoT Mtwara Bw. Lucas Mwimo

Mwenyekiti wa mafunzo ya siku tano ya Waandishi wa habari za Uchumi, Biashara na FedhaAbduel Elinaza akitoa neno la shukurani kwa uongozi wa BoT kwa kuhakikisha mafunzo hayo yanakwenda vizuri na kwa ufanisi mkubwa









Wanahabari mbalimbali wakichangia na kueleza ni kwa namna gani wamenufaika na mafunzo ya siku tano ya Uchumi, Biashara na FedhaWaandishi wa habari za Uchumi, Biashara na Fedha wakifuatilia yaliyokuwa yakijadiliwa ukumbini humo wakati wa kufungwa kwa Semina hiyo ya siku tano mkoani Mtwara.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2