RWEIKIZA ATOA MILIONI KUMI KATA KISHOGO NA KASHARU. | Tarimo Blog

Na Abdullatif Yunus Michuzi TV.

Dkt. Jasson Samson Rweikiza ameendelea na Ziara yake Jimboni ya kushukuru na Kutimiza ahadi alizozitoa kipindi cha Uchaguzi, sambamba na kuwasalimia Wapiga Kura wake.

Akiwa Njiani kuelekea Kata Kishogo, amepita Shule ya Sekondari Bujugo, Kata Bujugo na Kuwasalimia Walimu na Wanafunzi kisha kuchangia Laki Mbili za Sukari ya Uji, pamoja na Mipira miwili ya michezo, Huku Laki Mbili na Mipira Miwili ikitolewa kwa Wanafunzi wa Nyakibimbili Sekondari, na Elfu Hamsini na Mpira mmoja kwa Shule ya Msingi Katongo.

Dkt. Rweikiza akiwa Kivukoni Kyanyabasa ameendelea kusisitiza Juu ya Nia ya Serikali kubadilisha Kivuko hicho na kuleta Kivuko kingine kipya cha Kisasa, ombi ambalo tayari limekwisha anza kufanyiwa kazi, na akiongeza kuwa Serikali Ina mpango wa kujenga Daraja eneo Hilo, hivyo kimoja chochote Kati ya Daraja na Kivuko kipya kimojawapo kitangulia.

Kwa upande mwingine Mhe. Rweikiza amefanya Mikutano miwili  Kata Kasharu na Kata Kishogo ambapo amewashukuru Wananchi hao kwa kumchagua na kwa Shule ya Sekondari Kasharu amechangia Shilingi Milioni 5 Kuendeleza Ujenzi wa Sekondari hiyo ambayo Awali aliwahi kuchangia Shilingi Milioni Mbili. Shule hiyo pia ikiwa na  mchango mkubwa kutoka kwa Wafadhili Jamhuri ya watu wa Korea.

Mhe. Dkt Rweikiza amehitimisha Ziara yake ya Leo kwa kufanya Mkutano wake na Wananchi wa Kata Kishogo, ambapo kilio kikubwa ni Zahanati ya Kijiji.

Changamoto zilizowasilishwa kwenye Zahanati hiyo ni pamoja na Umeme, Wodi ya Wanaume na upungufi wa Wahudumu wa Afya.

Akijibu changamoto hizo kuhusu Umeme ametoa Milioni Tano na kusisitiza kuonana na Tanesco kwa ajili ya kutatua Kero hiyo, na huku akielekeza Mganga Mfawidhi kuacha kuwatoza malipo Akinamama Wajawazito Wazee na Watoto, huku Mganga Mkuu wa Wilaya akiahidi kushughulikia changamoto ya Ukosefu wa Wodi ya Wanaume kwa kuipeleka katika vikao vinavyoshughulikia bajeti ijayo, ili iwekwe katika mpango.

Muonekano wa Kivuko Cha Kyanyabasa kilichopo Jimbo la Bukoba Vijijini Mto Ngono, kilizinduliwa na Dkt. John Pombe Magufuli akiwa Waziri wa Ujenzi kwa Sasa likionekana kuchakaa licha ya kuendelea kutoa Huduma.
Dkt. Rweikiza akitazama uchakavu wa miundo mbinu ya Kivuko Cha Kyanyabasa ambacho kinavushaa wastani wa Abiria 200 na magari 20 kwa Siku.
Muonekano wa Zahanati ya Kijiji Kishogo ambayo inakabiliwa na Changamoto ya Umeme, Wahudumu na Wodi ya Wanaume kwa Sasa ikihudumia wastani wa wagonjwa 100 kwa siku, wagonjwa wengine wakitokea Vijiji Vya kata Jirani Kama Butainamwa-Kasharu na Kyabagenzi-Nyakibimbili.
Ukosefu wa Umeme kwenye Zahanati hii unapeleka kuzorota kwa Huduma na wakati mwingine kusababisha Vifo kadhaa, kutokana na Huduma husika zikiwemo kutunza damu na madawa.
Dkt Rweikiza akiongea na Wanafunzi Walimu na Wazazi wa Kata Kasharu na Sekondari Kasharu alipofika Katani humo kuwasalimia

Moja katinya Majengo Matatu ya Shule ya Sekondari Kasharu ambayo Ina mapungufu ya Jengo la Maabara, Ofisi ya Walimu, Madarasa na Matundu ya Vyoo.
 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2