Na Said Mwishehe, Michuzi TV.
KWA asilimia 100! Ndivyo unavyoweza kuelezea baada ya jina la Dk.Philip Mpango kuthibitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Makamu wa Rais.
Akitangaza matokeo ya kura ambazo zimepigwa na wabunge wote, Spika wa Bunge Job Ndugai amesema kuwa jina la Dk.Mpango limethibitishwa kwa asilimia 100 kwani wabunge waliopiga kura ni 363 na sasa anasubiri kuapishwa na Jaji Mkuu.
"Wabunge waliokuwepo humu ndani ni 363 na wote wamepiga kura ya ndio kuthibitisha jina la Dk.Philip Mpango kuwa Makamu wa Rais mteule wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Hivyo amethibitishwa kwa asilimia 100 ya kura ambazo zimemthibitisha.Kwa mujibu wa Katiba anasubiri kuapishwa,"amesema Ndugai.
Aidha amesema kuwa baada ya jina lake kuthibitishwa na Bunge, Katiba inaweka wazi kwamba jimbo la Buhigwe sasa liko wazi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi itaendelea na mchakato wa kutangaza rasmi ratiba ya uchaguzi mdogo kwa ajili ya kujaza nafasi hiyo ambayo imeachwa wazi baada ya Dk.Mpango jina lake kuthibitishwa na Bunge kuwa Makamu wa Rais.
Kabla ya kutangaza matokeo hayo,Spika Ndugai alimpa nafasi Dk.Mpango ya kuzungumza kwa mara mwisho ndani ya Bunge hilo kwani baada ya hapo hataruhusiwa kuzungumza chochote kwa mujibu wa Katiba.
Kabla ya kumkaribisha Dk.Mpango, Spika Nduga aliwaambia wabunge kwa mujibu wa Katiba jina lake likashapitishwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hataweza kuzungumza bungeni, hivyo ni vema akazungumza kabla ya jina kuthibitishwa na Bunge.
"Nimehangaika sana kupata jibu la nini tufanye, nimeangalia katiba yetu inaeleza wazi kabisa, hivyo tukisubiri athibitishwe na Bunge kisha aseme haitawezekana, hivyo azungumze kabla jina halijathibitishwa.Kuna watu huko nje huko wataanza kusema Spika hakufuata Katiba.Dk.Mpango karibu uzungumze na wabunge kwa mara mwisho humu ndani,"amesema Spika Ndugai.
Dk.Philip Mpango aliyethibitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Makamu wa Rais.Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment