*Ataja mambo atakayoanza nayo, awaaambia wabunge yeye si mpole...kuwabeba masikini
Na Said Mwishehe, Michuzi TV.
KABLA ya jina lake kuthibitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika nafasi ya Makamu wa Rais, Dk.Philip Mpango amepata fursa ya kuzungumza akitaja mambo kadhaa ambayo atahakikisha anayasimamia na kumshauri Rais Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza baada ya Spika wa Bunge Job Ndugai kumpa nafasi ya mwisho kuzungumza na wabunge maana akithibitishwa hataruhusiwa, Dk.Mpango amesema anamshukuru Mungu.
"Siku ya leo sina maelezo lakini naomba muendelee kunisaidia kushukuru Mungu pamoja nami, kwa miaka mingi nimekuwa kwenye nafasi mbalimbali.Nimekuwa nasumbuka sana na umasikini, kwasababu ile ile nimevaa kiatu cha umasikini toka utoto wangu, ndio maana hata nilipokuwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam nisilisoma uchumi wa maedeleo.
Inapofika siku hii ambayo wabunge mtanithibitisha katika nafasi ambayo Rais amependekeza, kazi yangu ya kwanza kumsaidia ni kuhakikisha ndoto ya watanzania inatimia.
"Sote ni mashahidi, nataka kukumbusha matukio mawili, wakati tunaomboleza, wananchi wanyonge kabisa kule Dar es Salaam waliruka fensi kwenda kumsikiza kipenzi chao Hayati Magufuli wakati mwili wake unataka kupakiwa kwenye ndege kuja DodomaTukio la pili nilishuhudia hapa Dodoma bodaboda walivyoamua kumsikindikiza kipenzi chao.
"Matukio haya mawili yanatoa ujumbe kazi ambazo zimeachwa na kipenzi chetu zisipokwenda vizuri hatuna namna, kwa hiyo tunatakiwa kuhakikisha ndoto za watanzania zinatimia, wanataka SGR yao ikamilike, wanataka bwawa la Mwalimu Nyerere likamlike, wanataka barabara na hasa za vijijini zikamilike.
"Wanataka huduma za afya ziwe bora zaidi, wanataka maji safi na salama, wanataka usalama wao waendeee kufanya shughuli zao.Hawataki rushwa, nachotaka kusema kama Bunge litanithibitsha haya ndio mambo nitakayokwenda kumsaidia Rais wetu ili nchi yetu isonge mbele, kiu ya wananchi itimie.Bunge ni chombo muhimu sana na katika miaka mitano na kidogo nimejifunza sana.
"Spika nataka nikushukuru wewe binafsi, mtangulizi wako alikuwa spika wa viwango, nadhan wewe ni Spika wa kidigital, umekuwa kiongozi mahiri, ukifika msimamo ni msimamo, mambo ya msingi lazima tusimamie, umeendesha Bunge hili vizuri licha ya kuwa na pande mbili,"amesema Dk.Mpango wakati anaaga Bungeni.
Aidha amempongeza Naibu Spika Dk.Tulia Ackson kwa jinsi anavyotekeleza majukumu yake ndani ya Bunge kwani amekuwa mwanamke shupavu na imara wakati wote."Waziri Mkuu una namna nyingi za kukuelezea, wakati wa hotuba sikutarajia kila alipozungumza alikuwa anasema mawaziri wenzangu ahsante kwa unyenyekevu.
"Wabunge hawa wakinipitisha nitajifunza kwako unyenyekevu, najua ulikuwa uhalili ili kumsaidia Rais na Makamu wa Rais katika kufanya kazi ambazo wakubwa wetu walikuwa wanakutuma, umekuwa darasa.Nawashukuru Kamati za Bunge, nimeshuhudia ushirikiano mzuri kati ya Wizara yangu na kamati zote, ahsanteni sana maana hiyo ndio inatupasa.Kazi hizi tufanye kwa uaminifu kabisa.
"Na mimi mkinithibitisha naomba Mungu anisaidie yale ambayo yatashauriwa na Bunge nitamshauri Rais yatekelezwe.Mimi ni binadamu najua kuna mengine hamkusema, kama nilimkwaza mtu yoyote naomba mnisamehe, na mimi sitatoka kabisa na lalamiko lolote juu ya mbunge yeyote.
"Najua mmesema mimi ni mpole, mcha Mungu, najitahidi maana bila yeye mimi si chochote.Muwe mnasema ukweli mimi sio mpole kiasi hicho, kwenye mambo ya hovyo hovyo sio mpole, kwenye mambo ya ubadhirifu wa fedha za umma mimi sio mpele, kwa watu wanaokula rushwa mimi sio mpole.
"Naomba mnisamehe, pale ambapo nitatakiwa kusimamia mambo kwa maslahi ya umma nitamshauri rais twende sawa, umasikini katika nchi yetu ni mkubwa, watu zaidi ya milioni 14 wanaishi chini ya kiwango cha umasikini, hii haiwezekani.Kwa hiyo wale ambao wanadokoa fedha za umma wale ni halali yangu.Naomba Mungu nisiwe na chuki na mtu yoyote wala nisionee yoyote,"amesema Dk.Mpango.
Ametumia nafasi hiyo kutoa ombi kwa wabunge wote kusimama imara katika kupigania maslahi ya Taifa huku akitoa ujumbe kwa wabunge wa upinzani kuhakikisha kwenye maslahi ya nchi wanatoa ushirikiano.
"Niseme ukweli nilikuwa naumia sana ninapowasilisha bajeti kwa ajili ya kusaidia wananchi masikini, wapinzani wanakaataa.Naomba tuwe wamoja, na pale ambapo kuna mambo ya msingi msisite simameni imara kuyasemea."
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment