BENKI ya CRDB Tawi la Mtwara limeanzisha programu ya kutoa mafunzo kwa akina mama wajasiriamali ili kuwawezesha kutambua changamoto na fursa katika kukuza mitaji ya biashara zao.
Programu hiyo ilianza hapa wiki iliyopita ambapo wanawake 300 kutoka makundi mbalimbali ya akina mama wajasiriamali walipatiwa mafunzo hayo huku benki hiyo ikiahidi kufikia akina mama wengi zaidi.
Meneja wa Tawi la CRDB Mtwara Anold Lwamtoga alisema programu hiyo ambayo pia ililenga kuadhimisha siku ya Mwanamke Duniani itasaidia wanawake wajasiriamali kurasimisha biashara zao, na kuwapatia mitaji.
“Leo tumewaleta pamoja akina mama 300 kuweza kuwandaa kupitia programu hii ili kujitambua kwanza kwenye Nyanja zao za biashara wanazofanya,” alisema Meneja huyo.
Alisema wanawakehao watafundishwa namna ya kuweza kutunza fedha vizuri kwa kufungua akaunti ya Malkia kwa benki ya CRDB bure.
“Lakini kupitia hiyo malkia account wanaweza pia wakapta mikopo mpaka ya asilimia 14 riba,,,riba ambayo tumewekea akina mama lakini kupitia akaunti hiyo wanaweza wakapata kwa kiasi cha amana ambacho wanacho kwa 90 per cent, kama ulikuwa milioni moja basi unaweza kukopa mpaka laki tisa,” alisema.
“Na hii yote tunafanya akina mama kujua kwamba hii ndio bank ambayo iko karibu na wao na ni yao na ndio benik ambayo inaweza kutatua changaoto zaa,” aliongeza.
Alisema benki hiyo imeona akina kwa makundi ambayo wanayo na uwezo wa biashara zao na uhitaji wanaweza pia kukopa mpaka shilingi bilioni tatu kuazisha laki mbili kulingana na mtaji wao na uwezo wa kusimamia biashara zao.
“Tunaona kwamba haya makundi ya akina mama yanakuja kutoa majibu kwenye jamii. Kwa sababu tumeona kuna wimbi kubwa la vijana ambao hawana ajira, hata ukimwezesha mama mmoja akawa na baishara yake ataajiri hata hao wasomi ambao wanatoka vyunoni,” alisema.
“Sasa sisi kama benki ni sehme yetu kubwa ya kuweza kusuma kurundumu hili la akina mama ili tuweze kubadilsiha uchumi wa Mtwara, kubadilisha uchumi wa mwanamke mmoja mmoja,” aliongeza.
Mwanamke mjasiriamali wa kukikundi cha akina mama wa usafi wa mazingira Wilayani Mtwara akitoa neno la shukran Kwa benki ya CRDB Tawi la Mkoa Kwa kuwawezesha vifaa vya kufanyia kazi katika shughuli zao za biashara.Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment