FCC KUENDELEA KUTOA ELIMU KWA WADAU KUTAMBUA UMUHIMU WA MATUMIZI ENDELEVU NA HUDUMA | Tarimo Blog

Na Janeth Raphael

TUME ya Ushindani nchini (FCC) imesema itaendelea kupeleka elimu kwa Wadau wa Uchumi wakiwemo wazalishaji, wasambazaji, wauzaji wa bidhaa na huduma kuwaelezea haki na wajibu wao katika kutambua umuhimu wa matumizi endelevu ya bidhaa na huduma yanayolinda mazingira.

Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mkuu wa TUME hiyo, Dkt. John Mduma alipokuwa akizungumzia maadhimisho ya Wiki ya haki za mlaji duniani kitaifa mwaka 2021.

Maadhimisho hayo hufanyika kila mwaka, March 15 ambapo Dkt. Mduma ametumia siku hiyo kuelezea hatua mbalimbali ambazo zinachukuliwa na FCC katika kutoa elimu kwa umma na kwamba TUME hiyo imeanzishwa kwa muhimu wa Sheria ya Ushindani No. 8 ya mwaka 2003.

Amefafanua ili kusimamia ushindani wa haki katika uchumi wa soko na kumlinda mlaji dhidi ya mienendo kandamizi na hadafu katika soko. Aidha amesema FCC imefanya maadhimisho ya wiki ya haki za mlaji ulimwenguni Kitaifa kwa kupeleka elimu kupitia vyombo mbalimbali vya habari katika majiji ya Dodoma na Dar es Salaam.

“Maadhimisho hayo yalianza March 11 na kilele March 15, Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya mlaji kwa mwaka 2021 inasema kukabiliana na uchafuzi wa mazingira unaletwa na taka za plastiki”, amesema Dkt. Mduma.

Hata hivyo amesema itakumbukwa Serikali imeshaanza hatua muhimu za kupiga vita mifuko ya Plastiki hatua kwa hatua, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira imeshapiga hatua kubwa katika udhibiti wa taka za Plastiki nchini.

Amesema Ofisi hiyo tayari imekamilisha awamu ya kwanza ya uondoshaji wa matumizi ya Mifumo ya Plastiki kufikia May 31, 2019. Mwitikio wa marufuku umefanikiwa kwa asilimia 100 ambapo sasa Mifumo mbadala ya vitambaa sambamba na vibebea vingine vinatumika kama vibebeo mbadala.

Aidha FCC imekusanya maoni na mapendekezo kutoka kwa Walengwa wa elimu hiyo ikiwa ni pamoja na mapendekezo ya hatua pendekezo za kukabiliana taka za plastiki na kwamba kama hayo ni muhimu kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha ukuaji endelevu wa uchumi na viwanda unazingatia utunzaji wa mazingira ili Jamii iwe na afya na ustawi.

 Mkurugenzi Mkuu wa TUME  ya FCC  Dkt. John Mduma 


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2