HATIMAE MGOGORO WA KIWANJA CHA PAPU WAMALIZIKA ,WAZIRI AKABIDHI HATI | Tarimo Blog



Waziri wa Mawasiliano Teknolojia ya Habari Dkt.Faustine Ndungulile akimkabidhi hati ya Ardhi Katibu mkuu wa Umoja wa Posts Afrika ,Katibu Mkuu wa umoja wa Posta Afrika (PAPU),Djibrine Younouss,kulia kwake ni Posta masta mkuu Hamisi Mwang'ombe.
Waziri wa Mawasiliano Teknolojia ya Habari Dkt.Faustine Ndungulile akikagua hati ya kiwanja Cha PAPU Mara baada ya kukabidhiwa na kwa niaba ya Katibu mkuu
Kaimu  Katibu mkuu wa Wizara ya  Mawasiliano Injinia Clarence Ichekweleza akimkabidhi Waziri wa Mawasiliano Teknolojia ya Habari Faustine Ndungulile hati ya kiwanja Cha PAPU leo Jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi Victor Nkya akitoa taarifa ya mradi wa makao makuu ya PAPU mbele ya Waziri wa Mawasiliano Teknolojia ya Habari Dkt.Faustine Ndungulile


Na Vero Ignatus,Arusha

Hatimae mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka 25 baina ya (PAPU) na baadhi ya wananchi wa kiwanja cha Makao makuu ya Posta Afrika kilichopo Mkoani Arusha umetatulika baada ya kukabidhiwa hati rasmi kwa umiliki kwa PAPU  kuwa Mmiliki halali wa kiwanja hicho.

Akizungumza katika makabidhiano hayo ya hati Waziri wa Mawasiliano Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndungulile alisema hii Ni moja ya mafanikio makubwa ya kukabidhi hati na hatujawahi kutokea katika Jiji la Arusha na utaleta tija .

Amewataka wakandarasi kuongeza kasi ya ujenzi huo kwnai wapo nyuma kwa wiki mbili ambapo amesema anaimani kuwa ifikapo June mwakani jengo hilo litakuwa limekamilika 

"Niwasihi  wakandarasi mnaosimamia mradi huu muhakikishe unamalizika kwa wakati kama ilivyopangwa mwezi wa sita ,2022 hivyo mhakikishe mnafanya kazi usiku na mchana ili umalizike kwa muda uliopangwa na kw wakati sahihi "
amesema Dkt.Ndungulile

Amesema kuwa, kukamilika kwa mradi huo kutaongeza ufanisi mkubwa katika utendaji kazi wao huku ikitoa fursa mbalimbali za ajira pindi jengo hilo litakapokamilika.

Amesema kuwa ,mradi huo hadi kukamilika utagharimu kiasi cha shs 33.6 bilioni , ambapo aliipongeza wizara ya ardhi kwa kufanya kazi nzuri ya kukabithi hati  hiyo kwani kwa muda mrefu walikuwa hawana hati ya kiwanja hicho.

Dkt.Ndungukile amelitaka Shirika la Posta  kuwa kielelezo pekee cha maendeleo ambacho kitakuwa mfano bora wa kuigwa huku akiwataka kwenda na kasi mpya ,na kuhakikisha makao makuu ya posta yanafafana huduma wanazotoa katika kuhakikisha inaendeshwa kidigitali zaidi.

Naye Mwenyekiti wa bodi kutoka TCRA,Dokta Jones Killimbe amesema kuwa,ujenzi wa jengo hilo ambao ndio utakuwa makao makuu ya posta Afrika na ofisi za Kanda ya kaskazini za PAPU ni ushindi  mkubwa Sana kwao kwani unaongeza ajira kwa watanzania walio wengi pia.

Dkt. Kilimbe amesema kuwa,uwepo wa jengo hilo utaongeza tija kubwa kwa mapato ya  fedha za kigeni pamoja na kuwepo kwa mikutano yote ya Kimataifa ambapo  ukumbi utakuwa na uwezo wa kubeba zaidi ya watu Mia tano .

Tunashukuru sana kuongezewa eneo kwani lililokuwepo lilikuwa dogo Sana ila kwa Sasa hivi eneo limepanuliwa  na kuwa kubwa ,hivyo tunashukuru Sana kwa serikali kwa ushirikiano mkubwa katika kukamilika swala hilo.”amesema.

Naye Katibu Mkuu wa umoja wa Posta Afrika (PAPU),Djibrine Younouss amesema kuwa,anashukuru Sana serikali kwa kuwapatia hati hiyo baada ya kuwepo kwa mgogoro kwa takribani miaka 25 Sasa na hivyo hivi Sasa umeweza kufikia mwisho na kuweza kupatiwa hati hiyo.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2