KENYATTA AMUENZI JPM KIIMANI | Tarimo Blog

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wakati akihutubia kwenye shughuli ya Kitaifa ya Kuaga Mwili wa Hayati Dkt John Magufuli, shughuli Iliyofanyika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Mwanafunzi Hassana Athuman Hassan wa Chuo cha Daarul Maarf cha Jijini Dodoma ambaye ametoa Adhana na kusababisha kusitishwa kwa Hotuba ya Rais Kenyatta
Msikiti wa Gaddafi ulipo Jijini Dodoma ambapo Adhana ilisikika kutokea Msikiti huo

*Asitisha Hotuba yake Kupisha Adhana.

Na Abdullatif Yunus Michuzi TV.
KATIKA Hali isiyotarajiwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Kenyatta amelazimika kusitisha Hotuba yake kwa Muda ili Kusikiliza Adhana iliyokuwa ikitolewa ikitolewa wakati wa Mchana Jirani na Ulipo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma wakati wa Tukio la Kitaifa la kuaga Mwili wa Hayati Dkt. John Magufuli likiendelea.

Tukio hilo ambalo kiimani lina uzito Mkubwa kwa Dini ya Kiislamu limeonekana kuwa gumzo kwa waliowengi kutokana na Rais Uhuru Kenyatta kiimani yeye ni Mkristo lakini ameheshimu Adhana hiyo kwa kunyamaza ghafla kwa muda ambapo kabla ya kufanya hivyo alitamka neno "Mwito" Hali hiyo ikitafisiriwa na jinsi gani Dini zinavyoheshimiwa hapa Nchini Jambo ambalo Hayati Magufuli alilisitiza.

Adhana hiyo iliyosikika kutoka Msikiti wa Gaddafi Dodoma Jirani na Uwanja wa Jamhuri, ambapo Kisheria katika Dini ya Uislamu inaelezwa kuwa, inaposikika Sauti hiyo yafaa kufuatisha maneno Yale ya muadhini au Kama huwezi kuyatamka vyema kukaa kimya.

Adhana likiwa Ni neno litokanalo na lugha ya Kiarabu lenye maana ya Tangazo au Wito, ni Sauti itolewayo kwa ajili ya WITO wa Swala, ikiwa na maana ya kuwaita waumini wa Dini ya Kiislamu kwenda kumlingania Mola wao Mtukufu, ikiwa Adhana hutolewa nyakati tofauti alfajiri, adhuhuri, alasiri, Magharibi, na Usiku.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2