Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Simiyu Emmanuel Silanga akizungumza mkoani Simiyu wakati wa Misa aliyoiandaa maalumu kwa Chama cha CCM mkoani Simiyu kumuombea Hayati Dk John Magufuli aliyekuwa Rais wa Tanzania jana.
PICHA NA MPIGAPICHA WETU
KATIKA ibada hiyo ambayo ilihudhuriwa na wananchi, watendaji wa serikali na wanachama wa CCM wakiongozwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Nec, Emmanuel Gungu.
Akizungumza katika ibada hiyo, Gungu alisema Hayati Rais Magufuli amefanya kazi kubwa hasa katika kuwaletea maendeleo ya Wananchi.
"Hapa Simiyu Hayati Rais Magufuli amefanya Mambo mengi. Ametujengea barabara za lami, miradi mikubwa ya maji Pamoja Na viwanda."Alisema Gungu.
Nae Katibu wa CCM Mkoa Wa Simiyu, Hawra Kachwamba alisema Watanzania wanapaswa kumueni Dk Magufuli kwa Mambo mengi mema aliyofanya kwa Watanzania.
Shekhe Mkuu wa Mkoa Wa Simiyu Mahamud Kalokola alisema Hayati Rais Magufuli alifanya mengi hasa kwa Watu wanyonge ambao kwa kiasi kikubwa alikuwa akiwatetea.
"Hayati Rais Magufuli amefanya Mambo makubwa, alikuwa mtetezi wa wanyonge. Kikubwa tumuombe huko aliko mungu ampunguzie adhabu ya kaburi."Alisema Shehe Kalokola.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga alisema Hayati Rais Magufuli alijipambanua kuwa mtetezi wa wanyonge na kwamba ni vema Watanzania wakaendelea kunuenzi na kumkumbuka kwa mema aliyoyafanya.
Ibada hiyo maalum ilifanyika katika Viwanja vya CCM Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu Na kwamba iliandaliwa na Chama Cha Mapinduzi.
Aidha, Viongozi wa dini wakiwemo wa Kanisa Katoriki, KKKT, Kanisa la Halisi la Mungu Baba, Kanisa la Wasabato.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment