Kampuni ya uzalishaji wa Sukari ya Kilombero inatarajia kutumia zaidi ya shilingi bilioni 584 za kitanzania kwa ajili ya ujenzi na upanuzi wa kiwanda hicho Mkoani Morogoro ujenzi utakaoanza Mwezi Mei Mwaka huu pindi taratibu zitakapokamilika shughuli itakayochukua miaka miwili na miezi mitatu.
Kampuni hiyo ambayo imekuwa ni tija ya kiuchumi kwa Wakulima wadogo wadogo kwa sasa ina wakulima elfu 66 wa zao la miwa wanaofanya kazi na kiwanda cha uzalishaji wa Sukari ambao wanazalisha tani 550,000 mpaka tani 600,000 kwa mwaka, kwa msimu mwaka 2018/2019 pekee walitoa tani za 629,000 na kulipwa kiasi cha shilingi bilioni 65 za kitanzania.
Akizungumza katika ziara hiyo, Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Dkt. Maduhu Kazi amesema utekelezaji wa upanuzi wa mradi huo ni swala ambalo ni la kushirikiana.
Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania Dkt. Maduhu Kazi .
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment