KITUO CHA MSAADA WA KISHERIA CHATOA ELIMU KWA VIONGOZI WA SERIKALI ZA MTAA KIGAMBONI | Tarimo Blog

ILI kuhakikisha kesi ambazo hazina msingi hazifiki mahakamani, Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC) kimeanza kutoa mafunzo kwa msimu wa pili kwa viongozi wa serikali za mtaa kati ya Vijibweni Kigamboni 

Akizungumza wakati wa kutoa Mafunzo ya Sheria za kazi na ajira kwa viongozi wa serikali za Mtaa na waajiriwa wa utumishi wa Umma, Wakili Zaituni Bwana amesema kuwa migogoro mingi ya wafanyakazi na waajiri yanapelekwa mahakamani pasi kujua kama yanaweza kumalizwa katika mabaraza ya serikali mtaa na kata.

Amesema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuondoa migogoro ambayo ipo kati ya waajiri na waajiriwa kwani kila mmoja akijua haki na wajibu wake na akizingatia kufanya katu migogoro ya waajiri na waajiriwa haita kuwepo au itapungua kufikishwa mahakama.

"Lengo kuu ni kutoa elimu juu ya sheria ya kazi na ajira za wafanyakazi makazini." Amesema Zaituni

Ikimbukwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alizungumza Machi 28, 2021 wakati akipokea Taarifa kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na rushwa (TAKUKURU) kuwa kesi zisizo na uhalali zipunguzwe kufika mahakamani.

Licha ya hilo Zaituni amesema kuwa kama kila mtu ikimfikia elimu ya sheria ya kazi na ajira itawezekana kabisa migogoro kuishia katika sehemu za kazi kwani elimu hiyo inaelekeza sehemu za kupeleka malalamiko ya Mwajiri na Mwajiriwa katika eneo husika.

"Tumeanza na viongozi wa serikali za mtaa pamoja na Watumishi wa Umma kwani wao wataweza kuwafundisha watu wengine kwa urahisi kwani wao ndio mara nyingi wanakutana na wanchi kwa wingi kwa hiyo wao watakuwa wa kwanza kusuluhisha kesi za waajiri na waajiriwa." Amesema Zaituni

Kwaupande wake Afisa Sheria kutoka Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC), Barcoal Deogratius amesema kuwa Mradi wa Kuiwezesha jamii kuijua sheria ya kazi na ajira ambao unatekelezwa kwa miaka miaka miwili ingawa kwa wanaenda kutamatisha mwaka huu wameona viongozi wa serikali za Mtaa wanachangia kwa kiasi kikubwa kutoa elimu ya haki za mwajiri na mwajiriwa.

Hata hivyo Deogratius amesema kuwa watu mirejesho mingi wanayoipata wakati wa utoaji wa elimu ya sheria ya ajira ni migogoro ya wafanyakazi wa kazi wa majumbani wao ndio wahanga wa migogoro ya waajiri na waajiriwa kwa hiyo kwa kutoa elimu hiyo kwa viongozi wa serikali ya mtaa watakwenda kusuluhisha.

Naye Mshiriki wa mafunzo hayo, Zainabu Mgandi Mwanyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kibena Kata ya Vijibweni amesema kuwa mafunzo ameyafurahiya kwani alikuwa hajui mambo ya kisheria sasa watakwenda kuisaidia jamii kwa kutatua migogoro inayohusiana na kazi na Sheria kwa urahisi.

Kwa Upande wa Afisa Sheria kutoka Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC), Rodger Michael akizungumza wakati wa kutoa mafunzo ya Sheria za Kazi na Ajira amesema kuwa sheria ya ajira na kazi inamruhusu mfanyakazi kuwa na likizo ya ugonjwa na likizo ya uzazi hata wafanyakazi wamajumani wanajumuishwa lakini hawa ndio wahanga zaidi.

Ameongeza kuwa kila mfanyakazi anatakiwa kuwa na likizo kwa mujibu wa sheria hiyo itawasaidia viongozi wa Serikali za mtaa kujua namna ya kutatua migogoro inayolingana na sheria hiyo.     
Wakili Zaituni Bwana akizungumza wakati wa kutoa mafunzo kwa viongozi wa serikali za mtaa katika kataa ya vijiweni Kigamboni mkoa wa Dar es salaam.
Afisa Sheria kutoka Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake (WLAC), Rodger Michael akizungumza wakati wa kutoa elimu  ya sheria ya ajira  na kazi kwa viongozi wa serikali za mtaa wa vijibweni.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2