NENDA RAIS MAGUFULI...NENDA MZEE WETU,MAUMIVU ...UMETULIZA WENGI | Tarimo Blog

 

TAIFA la Tanzania linalia,Watanzania wanalia, Afrika Mashariki inalia,Afrika inalia na Dunia inalia baada ya kutolewa taarifa za kufariki dunia kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Joseph Magufuli amefariki dunia.

Ni pigo,tena pigo kubwa , Rais Magufuli kipenzi cha Watanzania ameondoka wakati ambao Taifa linamuhitaji.Kwanini umetuacha mapema kiasi hichi, kwanini baba? 

Tulikupenda,tunakupenda na tutaendelea kukuenda.Ni kweli umetuacha lakini kwa uliyoyafanya kwa nchi yetu utaishi kwenye mioyo yetu daima.

Wakati naelezea haya naomba nieleze ugumu uliopo unapotaka kumuelezea Rais Dk.John Pombe Joseph Magufuli, ninajipa ujasiri alau ninachokisema kieleweke kwa Watanzania ambao kwa sasa wote tuko kwenye.majonzi na masikitiko makubwa.

Kabla ya kumuelezea Rais Magufuli naomba tuanze kukumbusha taarifa rasmi iliyotolewa kwa umma na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan kupitia Televisheni ya Taifa (TBC) usiku Machi 17, 2021 saa 5 usiku.

Wakati anatangaza kifo cha mpendwa wetu, Makamu wa Rais alisema hivi imeeeza kuwa Rais Magufuli amefariki dunia leo kwa maradhi ya Moyo akiwa katika Hospitali ya Mzena jijini Dar. Rais Magufuli alilazwa tarehe 6 Machi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa tatizo la moyo wa mfumo wa umeme.

Nchi itakuwa katika kipindi cha maombolezo kwa siku 14 na bendera zitapepea nusu mlingoti.

Kama kuna siku mbaya na ngumu ambayo Watanzania hatutasahau basi ni Machi 17 ya mwaka 2021.Taarifa za kifo cha Rais Magufuli kimetufanya Watanzania tukose nguvu,tukose la kusema, tumebaki tunalia, tumebaki na maumivu moyoni.


WASIFU:

Dkt, John Joseph Pombe Magufuli ni mwalimu na mtalaamu wa kemia akiwa na Shahada ya Uzamivu (PhD).

Kuzaliwa

Alizaliwa Oktoba 29 mwaka 1959 huko Chato mkoani Geita, Kaskazini magharibi mwa Tanzania

Elimu

Magufuli alipata elimu ya msingi katika shule ya msingi Chato kuanzia mwaka 1967 hadi 1974.

Mwaka 1975 alijiunga na Seminary ya Katoke iliyo Biharamulo, Kagera kwa Elimu ya sekondari na kisha kujiunga na shule ya sekondari ya Lake iliyoko Mwanza hadi 1978 alipohitimu.

Mwaka 1979 alijiunga na shule ya Sekondari ya Upili ya Mkwawa, Iringa kwa ajili ya masomo ya kidato cha tano na sita na kuhitimu Mwaka 1981.

Mwaka 1981 hadi 1982 alisomea Stashahada (Diploma) ya Ualimu wa masomo ya Sayansi katika Chuo cha Ualimu cha Mkwawa, Iringa Masomo makuu yakiwa Kemia na Hisabati

Akiwa kazini, Magufuli aliamua kujiendeleza kwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) mwaka 1985 hadi 1988 alipotunukiwa Shahada ya Ualimu katika masomo ya Kemia na Hisabati.

Mwaka 1991 hadi 1994 alisomea Shahada ya Uzamili ya Kemia (Msc. Chemistry) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Tanzania na Chuo Kikuu cha Salford, Uingereza.

Mwaka 2009 alitunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Kemia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Mafunzo ya Kijeshi

Kati ya Mwaka 1983 na 1984, Magufuli alipitia mafunzo ya kijeshi kwa mujibu wa sheria kwenye Kambi za Jeshi la Kujenga Taifa Makutupora - Dodoma, Makuyuni - Arusha na Mpwapwa - Dodoma.

Kazi

Baada ya kufuzu Stashahada ya Ualimu, alifundisha masomo ya Hisabati (Mathematics) na Kemia (Chemistry) katika shule ya Sekondari Sengerema kuanzia mwaka 1983.

Baada ya hapo akafanya kazi kama Mkemia katika Chama cha Ushirika cha Nyanza huko Mwanza hadi mwaka 1995.

Siasa.

Nyota ya Magufuli liana kung’aa katika siasa, alipogombea na kushinda ubunge eneo la Chato mwaka 1995. Mwaka huo huo aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi, nafasi aliyohudumu hadi Mwaka 2000.

Baada ya uchaguzi Mwaka 2000, aliteuliwa kura Waziri wa Ujenzi, nafasi aliyohudumu hadi Mwaka 2006 alipohamishwa kwenda Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi alipokaa hadi Mwaka 2008.

Mwaka 2010, aliteuliwa kawa Waziri wa ujenzi kwa mara ya pili na kudumu kwenye nafasi hiyo hadi Mwaka 2015.

Urais

Mnamo Tarehe 12 Julai 2015, alichaguliwa kuwa mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Akiwa na Samia Suluhu Hassani kama mgombea mwenza.

Tarehe 29 Oktoba 2015 alitangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ushindi wa kura 8,882,935 sawa na 58.46%.

Magufuli aliapishwa kama Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 5 November 2015.

Muhula wa Pili

Mnamo tarehe 30 Oktoba 2020, Tume ya Uchaguzi Tanzania ilimtangaza John Pombe Magufuli kama rais kwa muhula wa pili kwa kupata kura milioni 12.5 hiyo ikiwa ni sawa na asilimia 84 akiwa amemshinda mshindani wake wa karibu, Tundu Lissu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) aliyepata kura milioni 1.9.

Baadhi ya Nukuu zake:

"Ni nafuu wakuchukie... uonekane wewe sio Mwanasiasa mzuri (Unpopular) kwasababu sikuja kutafuta Mchumba. Nimekuja Kufanya kazi za Watanzania." - Septemba 7, 2017.

Pamoja na yote hayo ni jukumu letu Watanzania kuendelea kumuombea Rais wetu apate pumziko la milele. Itoshe kusemw Rais Magufuli ile kauli yako ya Hapa Kazi Tu tutaitekeleza kwa vitendo, tutaendelea kudumisha umoja,upendo na mshikamano kama ambavyo umekuwa ukituhubiria nyakati zote, ulitufundisha kujiamini, tukuahidi tutaendelea kujimini.

Wakati nahitimisha kumuelezea Rais Magufuli, naikumbuka miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu.Tulitarajia ushuhudie kazi nzuri uliyoanzisha 

Watanzania walitamani siku ya kuzinduliwa mradi wa kufua umeme wa Bwawa la Julius Nyerere uwepo, tulitamani wakati wa uzinduzi wa reli ya kisasa uwepo,tulimatani ujenzi wa miradi mikubwa uliyoanzisha wakati itakapokamilika uwepo.

Mungu muumba wa mbingu na ardhi amekuchukua.Basi baba nenda, nenda Rais wetu,nenda mzew Magufuli, hatutasahau watoto Watanzania kusoma bure kuanzia elimu ya msingi hadi kidato cha nne. Bwana ametoa,Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2