WAFANYABIASHARA WA UTALII ,MADINI WAMLILIA MAGUFULI ,WAHIDI KUMPA USHIRIKIANO RAIS SAMIA | Tarimo Blog
Na Woinde Shizza, Michuzi Tv -ARUSHA
Wafanyabiashara wakubwa na wadogo (machinga) wametakiwa kuendelea kulipa kodi kwa wakati ili kumuwezesha Rais Samia Hassan Suluhu kuendelea kutekeleza miradi yote na kazi zote zilizoachwa na hayati John Magufuli.
Aidha wafanyabiashara wa madini wasitoroshe madini ,wakifanya hivyo wanapoteza mapato ya nchi ambayo fedha zinazopatikana zitasaidia kuendeleza miradi ya maendeleo iliyoachwa na hayati Magufuli.
Hayo yamebainishwa na mfanyabiashara wa utalii na madini Samweli Rugamalila wakati akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo ya hayati Magufuli nje ya viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha, ambapo alisema katika kipindi Cha hayati , wananchi walikuwa wakilipa kodi vizuri bila ubabaishaji hivyo ni vyema wakaendelea kulipa hivyo hivyo ili kumuwezesha Rais wa Sasa kupata fedha za kuendeleza miradi iliyoachwa.
Alisema kuwa hayati Magufuli alikuwa na malengo ya kufikisha nchi ya Tanzania mbali ambapo alibainisha kunamiradi mingi ambayo alianzisha na ajaimaliza inatakiwa kumalizika kama vile miradi treni ya umeme ,ununuzi wa ndege ,mradi wa umeme wa mto rufiji(Steeler) pamoja na mingine mingi ambayo yote inaitaji fedha zitokanazo na ulipaji kodi ili imalizike.
Kwa upande wake katibu wa chama cha wachimbaji madini mkoa wa Manyara tawi la mererani Rachael Njau alisema kuwa wao Kama wachimbaji hawata mesahau hayati Magufuli kwani amewasaidia mengi ikiwemo kuwajengea ukuta wa mererani ambao umesaidia kwa kiasi kikubwa kuthibiti utoroshwaji wa madini.
Alisema wataendelea kumbuka kama mtetezi wa Tanzania ,kiongozi aliyepigania maendeleo ya watu wake na kupambana na rushwa na ufisadi ,hakuvumilia wateule wake waliofanya uzembe na kutowajibika.
Aidha pia alimpongeza Rais Samia Suluhu nakusema kuwa wao Kama wanawake wachimbaji wa madini wataendelea kumuunga mkono na kumuombea ili aweze kufikisha mbali nchi yetu ya Tanzania.
Mpaka wanja maarufu mkoani Arusha Raphael Nchimbi akitoa heshima za mwisho mbele ya picha ya aliekuwa Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli jana alipotembelea ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha kusaini kitabu cha maombolezo (picha na Woinde Shizza , Arusha).
Mfanyabiashara mkubwa wa matairi mkoani Arusha Valerian Shayo akisaini kitabu Cha maombolezo ya hayati Rais John Pombe Magufuli jana (leo) Katika viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha ambapo alisema Rais Magufuli ameacha pengo kubwa(picha na Woinde Shizza , ARUSHA )Mfanyabiashara wa utalii na madini Samweli Rugamalila akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo ya hayati Rais John Magufuli (picha na Woinde Shizza).
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment