MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR ASEMA MSIBA WA DK MAGUFULI SIYO WA TANZANIA PEKEE BALI UMEZIGUSA HADI NCHI NYINGINE | Tarimo Blog









Charles James, Michuzi TV

MSIBA wa Taifa! Ni kauli ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemedi Suleiman Abdullah ambapo amesema wingi wa watu wanaojitokeza katika vituo vyote ambavyo mwili wa aliyekua Dk John Magufuli unapita kwa ajili ya kuagwa na kupewa heshima za mwisho.

Makamu wa Pili Abdullah amesema hakuna mtanzania yoyote mwenye akili timamu ataacha kusikitika kutokana na msiba huo mkubwa uliolikumba Taifa kwa kuondokewa na kiongozi mahiri ambaye aliipenda Nchi yake.

Amesema Dk Magufuli alifanya kazi kubwa ya kuwatumikia watanzania wote bila kubagua na hakuna sehemu yoyote ambayo aliacha kuigusa na kuacha alama yake jambo ambalo limeifanya Nchi yetu kupata sifa kubwa ndani na nje ya Nchi.

" Hakuna sehemu ambayo hajaacha alama, amelitumikia Taifa kwa uzalendo mkubwa, siyo kwenye sekta ya madini, afya, elimu, miundombinu ya barabara, umeme na maji kote huko ameacha alama kubwa sana itakayoishi milele.

Siyo hivyo tu heshima ya Dk Magufuli itaendelea kukumbukwa milele na milele kwani alituinua kutoka kuwa Nchi yenye uchumi wa chini hadi kuwa Nchi yenye uchumi wa kati hata kabla ya muda uliokua umepangwa," Amesema Makamu wa Rais Abdullah.

Amesema msiba wa Dk Magufuli umepokewa kwa masikitiko makubwa hata na Nchi zingine na ushahidi wa jambo hilo ni idadi kubwa ya marais na viongozi waliokuja kwenye maziko ya kitaifa yaliyofanyika jijini Dodoma.

" Niwaombe watanzania tuendelee kuwa watulivu na zaidi tumuenzi mpendwa wetu kwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii, uaminifu na uzalendo mkubwa, nisisitize tuendelee kusimama Imara tushirikiane, tushikamane na tuendelee pale alipotuacha Dk Magufuli.

Juzi wakati mwili wa Dk Magufuli ukipitishwa kuagwa barabarani kwenye mitaa ya Zanzibar vijana walikua wakiusindikiza wakiimba nyimbo za Dk Magufuli, na baadae wakanitumia salamu kuwa wanataka kuendelea kuongozwa kama ilivyokua kwa Dk Magufuli, " Amesema Makamu wa Rais Abdullah.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2