WanamorogoroTutamuenzi Dkt Magufuli daima-RC Morogoro | Tarimo Blog


Na Farida Saidy, Morogoro

Wananchi Mkoani Morogoro wametakiwa kumuenzi Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kwa kudumisha, amani na upendo aliowaachia Hayati Dkt. Magufuli baada ya kumaliza migogogo kati ya wakulima na wafugaji iliyodumu kwa muda mrefu bila ya kupatiwa kufumbuzi.

Wito huo umetolewa Machi 23 Mwaka huu Wilayani Mvomero na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare wakati wa maombolezo ya Hayati Dkt. Magufuli ambayo yamefanyika Kiwilaya katika Ofisi za Wilaya ya Mvomero.

Akizungumza wakati wa maombolezo hayo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare,amesema moja ya kazi kubwa aliyopewa na Hayati Dkt. Magufuli wakati wa uteuzi wake ni kumaliza migogoro kati ya wakulima na wafugaji iliyokuwa ikiendelea katika Wilaya mbalimbali ikiwemo ya Wilaya ya Mvomero.

“Nashukuru Mungu tulipokutana ametoa pongezi za kutosha kwangu na kwa viongozi wote wa Mkoa wa Morogoro kwamba angalau kwa Mwaka mmoja tu tumeweza kuthibiti na kuhakikisha hawawezi kupata taarifa kubwa ya migogoro.” alisema RC Sanare.

Aidha, katika kumuenzi Dkt. Magufuli RC Sanare amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Bwana Albinus Mgonya kuhakikisha wanasimamia kikamilifu bila ya ubadhirifu mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari Sokoine, ambayo Hayati Dkt Magufuli alitaka ikamilike kwa wakati ili wanafunzi waanze kusoma.

Awali Katibu Tawala wa Mkoa huo Mhandisi Emmanuel Kalobelo mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kisha kuzungumzia namna ya kumuenzi kiongozi huyo.

‘’ Tunashukuru kwakweli tangu tumekuja hadi sasa migogoro ya Ardhi imepungua sana, viongozi katika ngazi mbalimbali wamejitahidi pamoja na sisi tumeshirikiana vizuri migogoro hiyo imepungua sana, sasa ili tumuenzi lazima hili tuliendeleze’’ Alisema Kalobelo.

Mhandisi Kalobelo amesema ili kufikia uchumi wa kati Mkoa huo hauna budi kuacha migogoro kati wakulima na wafugaji na kufanya kazi kwa bidii kwa kutumia rasilimali zilizopo kwa ajili ya kuongeza kipato katika familia zao na nchi kwa ujumla.

Sambamba na hayo, Mhandisi Kalobelo amewataka wananchi na viongozi kumuombea Rais wa Serikali ya Awamu ya Sita, Mhe. Samia Suluhu Hassan afya njema na maono makubwa ili nchi iendelee na kasi ileile, lakini pia kutoa ushirikiano wa hali ya juu ili mataifa ya nje yasione utofauti wa kutokuwepo kwa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro  Loata Ole Sanare akiwa KATIKA picha ya pamoja na viongozi wa Dini waliohudhuria katika maombolezo ya Hayati Dkt  John Pombe Magufuli.
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Bwana Albinus Mgonya Akiwaonesha picha ya Hayati Dkt John Pombe Magufuli kwaajili ya kumkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare.
Baadhi ya Waananchi walio hudhulia katika Maombolezo  ya Hayati Dkt John Pombe Magufuli, Wilayani Mvomero.

 
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2