Watano wa familia moja wazikwa leo Kimara huku mipango ya mazishi ya dada wa kazi ikiendelea. | Tarimo Blog

Na waandishi wetu, Michuzi TV
WATU watano wa Familia Moja waliofariki Machi 21 wakati wa kumuaga aliyekuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hayati Dkt. John Pombe Magufuli wamezikwa leo katika makaburi ya Familia yaliyopo Kimara Mkoani Dar es Salaam.

Aidha kwa mujibu wa familia ya Mtuwa, taratibu za kuuhifadhi mwili wa marehemu Anitha Mfikwa ambaye alikuwa dada wa kazi wa marehemu Suzan zinaendelea nyumbani hapo ambapo kwa sasa wanazungumza na wazazi wa marehemu waliopo mkoani Njombe na wale waliopo Mkoani Dar es Salaam ili kufahamu ni wapi watauhifadhi mwili wa mpendwa wao Anitha.

Maziko ya wanafamilia hiyo ya watu watano yamefanyika mida ya saa kumi jioni yakutanguliwa na ibada ya Ibada iliyofanyika katika Kanisa la KKKT Kimara Dar es Salaama na kuongozwa na Mchungaji wa kanisa hilo, Wilbard Mstai huku watu wengi wakihudhuria ibada hiyo.

Kabla ya Ibada ya kuwaombea marehemu hao ilitanguliwa na Salamu za rambi rambi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Masare Makori Pamoja na Mbunge wa Jimbo Kibamba Issa Mtevu.

Licha ya kutoa salamu za rambi rambi viongozi hao wa kiserikali pia waliwapa pole wafiwa na kuwasihi kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu.

Pia kulikuwa na salamu za pole kutoka kwa viongozi wa kanisa pamoja na wawakilishi wa shule ambazo watoto hao walikuwa wakisoma.

Baada ya Ibada hiyo wananchi waliweza kuaga miili ya watu watano wa Familia ya Mtuwa huku wakimalizia ndugu wa karibu wa familia hiyo na kuelekea katika makaburi ya Familia.

Waliofariki dunia na kupumzishwa katika Makaburi ya Mtuwa ni Susan Mtuwa na watoto wake wawili, Nathan (6) na Natalia (5) pamoja na watoto wengine wawili wa Shemeji zake ambao Michelle (8) na Christian (11) ambao ni watoto wa shemeji zake Susan huku dada wa kazi wa familia hiyo alipatikana amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Mkoa wa Dar es Salaam.
Makaburi ya wanafamilia watano waliofariki dunia Machi 21, 2021 katika Uwanja wa Uhuru wakati walipokuwa wameenda kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021.

Majeneza yenye miili ya wanafamilia watano waliofariki dunia siku ya kuaga Mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.
Wanafamilia wakiweka mashahada katika makaburi ya ndugu watano waliofariki dunia katika Uwanja wa Uhuru uliopo Temeka Mkoa wa Dar es Salaam.
Wanafamilia wakiweka mashahada katika makaburi ya ndugu watano waliofariki dunia katika Uwanja wa Uhuru uliopo Temeka Mkoa wa Dar es Salaam.
Wanafamilia wakiweka mashahada katika makaburi ya ndugu watano waliofariki dunia katika Uwanja wa Uhuru uliopo Temeka Mkoa wa Dar es Salaam.
Skauti akiwa amebeba moja ya msalaba wa moja wa wanafamilia watano waliofariki dunia Machi 21, 2021 katika Uwanja wa Uhuru ulipo Temeke Mkoa wa Dar es Salaam.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2