TAIFA STARS KUWAKABILI LIBYA BILA MASHABIKI JUMAPILI | Tarimo Blog


Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania ( TFF) limesema kuwa mchezo wa makundi kufuzu Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) dhidi ya Libya hautakuwa na mashabiki.

Taarifa iliyotolewa na TFF, imesema kuwa mchezo huo utakaochezwa Machi 28 dhidi ya Libya hautakuwa na  mashabiki baada ya kupokea barua kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF.)

Mchezo kati ya Taifa Stars na Libya utapigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam kuanzia sa 10  alasiri.

TFF wamesema kuwa, wamepokea maelekezo kutoka CAF kuwa katika mchezo huo hautakuwa na mashabiki.

Mbali na hilo, Timu ya Taifa nashuka dimbani usiku huu kuwakabili timu ya Taifa ya Equatorial Guinea katika mchezo wa makundi kufuzu Fainali za Mataifa Ya Afrika (AFCON.)

Mchezo hyo unaotarajiwa kupigwa saa 4 ya usiku kwa masaa ya Afrika Mashariki utapigwa katika nchi ya Equatorial Guinea.

Baada ya kukamilika kwa mchezo huo  Taifa Stars watarejea nchini kwa ndege ya kukodi ili kujiandaa na mchezo wa Jumapili dhidi ya Libya.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2