MAKAMU WA PILI WA RAIS ZANZIBAR AONGOZA WAKAZI WA GEITA NA MIKOA JIRANI KUMUAGA JPM | Tarimo Blog


Na Mwandishi Wetu, Geita

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdulah, amewaongoza wakazi wa Geita na mikoa jirani kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati John Pombe Magufuli katika uwanja wa Magufuli Chato mkoani Geita.

Akizungumza katika shughuli hiyo ya kuuaga mwili wa hayati Magufuli wilayani Chato, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa kamati ya mazishi kitaifa amewasihi Watanzania kuendelea kushikamana katika kulijenga taifa, ambalo Magufuli ameliacha salama na lenye heshima.

Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, amesema ni wajibu wa viongozi na Watanzania kuungana kuenzi mazuri yote aliyofanya Hayati Magufuli na kuendeleza sera zake za kuchapa kazi, kupiga vita rushwa na ubadhirifu na kuweka mbele uzalendo na maslahi ya taifa.

Mazishi ya Hayati Dkt. Magufuli yatafanyika Ijumaa Machi 26, 2021 katika makaburi ya familia kijijini kwake Chato mkoani Geita.


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdullah akiongoza wananchi kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Uwanja wa Magufuli kijijini Chato mkoani Geita leo Machi 25, 20121
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulah akizungumza na wananchi wakati wa tukio la kuaga mwili wa hayati Dkt. John Pombe Magufuli, kwenye uwanja wa Magufuli , Chato, Mkoani Geita Machi 25, 2021 .

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli Chato mkoani Geita


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akisaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chato kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli Chato mkoani Geita




Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akisaini kitabu cha maombolezo katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chato kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli Chato mkoani Geita

Mawaziri mbalimbali pamoja na viongozi waandamizi wa Serikali wakiwa katika uwanja wa Magufuli tayari kwa zoezi la kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli katika uwanja wa Magufuli Chato mkoani Geita

Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi-Zanzibar, Mhandisi Zena Ahmed Said akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge katika uwanja wa Magufuli wakati wa zoezi la kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli Chato mkoani Geita


Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Bashiru Ally akiteta jambo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) katika uwanja wa Magufuli wakati wa zoezi la kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli Chato mkoani Geita

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2