Emmanuel Bundala (aliyevaa koti jekundu) akiungana na watoto wanaoishi mitaani kula chakula cha mchana kilichoandaliwa na Kanisa la Pentekoste la PHAMT Bethania Dodoma kwenye viwanja vya Nyerere Square. Emmanuel ni mtoto wa Askofu Bundala ambaye alishiriki kuwatakusanya watoto hao pamoja maandalizi ya chakula hicho. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Watoto wanaoishi mitaani wakinawishwa mikono tayari kupata chakula
Na Richard Mwaikenda, Dodoma
Askofu Julius Bundala wa Kanisa la Pentekoste la PHAMT Bethenia Dodoma akiwahubiria watoto wanaoishi mitaani baada ya kula nao chakula cha mchana siku ya Jumatatu ya Pasaka kwenye viwanja vya Julius Nyerere jijini Dodoma. Baada chakula aliwahubiria kwa kuwataka kumrudia Yesu Kristo ili warudi kwenye hali yao ya kawaida badala ya kuishi maisha yasiyofaa mitaani.
Mdau, nakuomba uendelee kusikiliza/kuona kupitia clip hii ya video, Askofu Bundala, mwanaye Emmanuel wakielezea lengo la kuwasaka watoto hao na kula nao chakula pamoja na kuwahubiria neno la Mungu lakini pia utawasikiliza watoto wakielezea pamoja na mambo mengine na jinsi wanavyopatwa na maswahibu wanapoishi mitaani....![](https://blogger.googleusercontent.com/img/proxy/AVvXsEgzNbFK8yo61jlttwC19i8kSyCOh1-UJ-qCVY2lJ1kQB8jjpiOUoh6NPYqHu6zHwxuBvuj2Cq58H9ThuTh0cK8QevcG2RhNNg9Bjlky5SA4jhqjPdonhb2eS0KNfj-pFDdEqGHg-LmDzNV3q9QmMg=s0-d-e1-ft)
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment