Dada wa Balali anatafutwa na Mahakama | Tarimo Blog

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa hati ya kukamatwa kwa dada wa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu, Tanzania marehemu Daudi Balali,  Elizabeth Balali kwa kuruka dhamana na kukwamisha kuendelea kwa kesi inayomkabili kwa zaidi ya miezi mitano.

 Mshtakiwa huyo pamoja na mdhamini wake wameshindwa kufika mahakamani kwa kipindi chote hicho bila kuitaarifu mahakama.

Uamuzi huo umetolewa leo Aprili 27, 2020 na Hakimu Mkazi Mfawidhi Godfrey Isaya wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya mshtakiwa Elizabeth kusoma maelezo ya awali lakini imeshindikana kwa kuwa mshtakiwa huyo hakuwepo mahakamani.

Mapema Wakili wa Serikali Faraji Nguka alidai mahakamani  hapo kuwa, shauri hili leo lilikuka kwa ajili ya kumsomea mshtakiwa maelezo ya awali lakini wote yeye na mdhamini wake hawakufika hivyo aliiomba mahakama itoe hati ya kumkamata.
Hata hivyo, Hakimu Isaya alisema hati ya kukamatwa kwa mshtakiwa huyo ilishatolewa.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 26, 2021.

Awali Elizabeth alikuwa akikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi yaliyomfanya akae gerezani zaidi ya miezi sita kabla hayajafutwa na kusomewa mashtaka mapya ya kujipatia Sh milioni 25 kwa ulaghai.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka ya sasa Mshtakiwa huyo anadaiwa kati ya Oktoba 19 na Desemba 21, 2017 katika Mkoa wa Dar es Salaam alijipatia kiasi cha Sh milioni 25  kutoka kwa Dk Roderick Kisenge kwa njia ya ulaghai baada ya kujifanya anamuuzia eneo la mita za mraba 900 ambalo halijapimwa katika eneo la Boko Dovya Kinondoni wakati akijua eneo hilo si lake.

Mshtakiwa alikana mashtaka na mahakama ilikubali kumpa dhamana ambapo alidhaminiwa na mdhamini mmoja aliyesaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni tisa.



Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2