Na HERI SHAABAN
MKUU wa Wilaya ya Temeke Godwin Gondwe amezindua nyumba ya Mshindi wa kwanza wa mashindano ya kusoma Qurani Tukufu Afrika ambayo yanatarajia kufanyika April 25 mwaka huu.
Akizindua mashindano hayo Mkuu wa Wilaya, Gondwe alisema ni baraka kwa Wilaya hiyo mashindano ya 21 kufanyika ndani ya Wilaya hiyo
"Leo tumezindua nyumba ambayo itashindanishwa katika mashindano ya usomaji Qurani Afrika mgeni Rasmi anatarajia kuwa Rais wa Zanzibar Dkt.Hussein Mwinyi na Mgeni maalum Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa " alisema Gondwe.
Gondwe alipongeza Taasisi ya mashindano hayo Al Hikma Foundation kwa kuandaa mashindano hayo kila mwaka ya Qurani tukufu Afrika April 25 mwaka huu .
Alisema katika kuelekea maandalizi ndani ya Wilaya hiyo ulinzi Upo vizuri mashindano yatafanyika uwanja mkubwa na kurushwa na Vyombo vya habari .
Pia Mkuu wa Temeke alikabidhi bendera ya Taifa kwa washiriki kutoka Tanzania bara na Tanzania visiwani ambapo kwa Tanzania washiriki watatu
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Al Hikma Foundation ,ambaye ni Mwenyekiti wa mashindano hayo Shekh Nurdin Kishiki alisema nchi ambazo zinashiri 21 katika mashindano hayo ya 21 Afrika ambayo yanafanyika hapa nchini .
Shekhe Kishiki alisema. nyumba hiyo hipo Dar es Salaam Wilaya ya Temeke yenye thamani ya milioni 40 ambayo atapewa mshindi wa kwanza na mshindi wa pili atakabidhiwa milioni 12 na mshindi wa tatu milioni nane.
Alisema siku pia wataomba dua kuliombea Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na kumuombea Dua Rais Samia Suluhu Hassan Mwenyezi Mungu amfanyie wepesi katika ufanyaji wa kazi zake.
Aliwataja wadhamini wa mashindano hayo Benki ya watu Zanzibar ,Chanel ten ,Kampuni ya afya Mashindano hayo ni bure .
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Godwin Gonde akizindua nyumba itakayoshindaniwa katika mashindano ya kusoma Qur'aani Tukufu Afrika ,mashindano hayo yanatarajia kufanyika April 25 mwaka huu (kulia) Mkurugenzi wa Taasisi ya Al Hikma Foundation Sbekh Nurudin Kishkki (PICHA NA HERI SHAABAN)
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment