Ecobank Tanzania yatoa elimu kwa Wabunge kuhusu huduma za Kibenki | Tarimo Blog

 

Timu ya Masoko na Uhusiano ya Ecobank Tanzania ikiongozwa na Mkuu wa kitengo cha wateja binafsi, Salma Mkambara imetembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutoa elimu kwa Waheshimwa wabunge na wafanyakazi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu huduma za Kibanki zinazotolewa na Benki hiyo.

Mkuu wa kitengo cha Wateja binafsi kutoka Ecobank Tanzania, Salma Mkambara pamoja na Meneja Mahusiano wa wateja Maalum kutoka Ecobank Tanzania Jackline Nyangoe wakimsikiliza Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai aliokuwa anauliza maswali kuhusu huduma zitolewazo na Benki hiyo wakati wa kutoa elimu kwa wabunge na wafanyakazi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai akisoma moja ya vipeperushi vya Ecobank Tanzania alipotembelea banda la benki hiyo kwa ajili yakupata elimu kuhusu huduma za Kibanki zinazotolewa na Benki hiyo Bungeni Jijini Dodoma leo.
Mkuu wa kitengo cha Wateja binafsi kutoka Ecobank Tanzania, Salma Mkambara(kushoto) akizungumza na Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai(wa pili kushoto) pamoja na mbunge mwingine kuhusu namna Benko hiyo ilivyojipanga kuwafikia watu wengi hapa nchini wakiwemo wabunge. Wa pili kulia ni Meneja Mahusiano wa wateja Maalum kutoka Ecobank Tanzania Jackline Nyangoe
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai akiwa kwenye picha ya pamoja na maofisa wa Ecobank Tanzania mara baada kupata elimu kuhusu huduma za Kibanki zinazotolewa na Benki hiyo Bungeni Jijini Dodoma leo.



Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2