Na Said Mwishehe,Michuzi TV
UONGOZI wa Kampuni ya GSM Group umeweka wazi utaendelea kuwekeza katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni sehemu ya mkakati wao wa kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambayo imesisitiza itaendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji nchini Tanzania.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa maduka mapya ya mitindo yaliyoundwa maalum kuhudumia mahitaji ya watu kwa jinsi zote, umri wote na haiba zote, Ofisa Mtendaji Mkuu wa GSM Group Fatma Abdallah amesema wanajisikia fahari kuendelea kuwa kitovu cha kibiashara ambacho kimetoa na kitaendelea kutoa ajira ,kutengeneza fursa za kibiashara,kuchochea ndoto za wote wanaokuja na kuchangia uboreshaji wa biashara ndani ya Tanzania.
Fatma Abdallah amefafanua GSM Group wamefurahishwa na kauli ya Rais Samia ambaye ameendelea kuweka mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji na kwamba siku zote wamekuwa wakishirikiana na Serikali katika kuunga mkono juhudi za viongozi wakuu wa nchi kuhakikisha Tanzania inazidi kupiga hatua.
" Tutaendelea kuunga juhudi za Serikali yetu katika kuhakikisha GSM Group tunashiriki kikamilifu katika eneo hili la uwekezaji na kufanya biashara kama ambavyo tumekuwa tukifanya siku zote,"amesisitiza.
Akizungumzia uzinduzi wa maduka mapya yaliyopo kwenye jengo la Salamander Tower ambayo ni ya Babyshop,Splash,Max na Shoexpress yote yakiwa ndani ya jengo moja ,jengo jipya na la kisasa katika Mtaa wa Samora jijini Dar es Salaam amesisitiza inaonesha jinsi ambavyo GSM Group imeamua kuendelea kusogeza huduma karibu na wananchi.
Awali akizungumzia uzinduzi wa maduka katika jengo hilo la Salamander, Ofisa Biashara wa GSM Group Allan Chanjo amesema wanamshukuru Mungu kwa kuwapatia nafasi nyingine na ya kipekee kabisa kushuhudia uzinduzi mkubwa kabisa ambapo GSM Group kupitia GSM Retail wanafungua maduka mapya ya mitindo yaliyoundwa maalum kuhudumia mahitaji ya watu wote.
"Dhumuni na tumaini letu tulipoamua kufungua maduka haya ndani ya Salamander Tower sio tu kuwafanya watu waingie na kununua,bali nia yetu inaenda mbali kwa kuwa sehemu ya kitovu cha biashara ambacho kimeendelea kutoa ajira, kwani tumetoa ajira zaidi ya 3000 hadi sasa na kwa jinsi tunavyoendelea kuwekeza tutatoa ajira zaidi,"amesema Chonjo.
Aidha amesema kama biashara,faida na matokeo chanya ambayo wameyapata sio ya kwao peke yao bali ni ya sote, jamii na nchi kwa ujumla hasa wanapoanza safari mpya pamoja na Watanzania."Tunaamini tutaendelea kukua nanyi, tukishirikiana katika kila hatua."
Amesisitiza " Na kitu ambacho leo ningependa tutafakari pamoja ,kwenye uzinduzi huu ni Ujumbe wa maandishi (almaarufu text) .Ninaamini wote leo tumepokea na tumetuma text ,kwa kifupi kutumiana text imekua ni mtindo wa maisha na imebadili kabisa jinsi tunavyowasiliana, unaweza kusema kuna ujumbe unaotumwa na text kwa kila mmoja wetu katika maisha.
"Kina text kea mabosi zetu,wafanyakazi wenzetu na wafanyabiashara wenzetu, kuna text kwa wapenzi wetu zinazoambatana na viomoji vya makopakopa ,kuna text kwa marafiki zetu zenye majina ya utani na lugha mnayoielewa ninyi tu, kuna text kwa wanafamilia zinazotukumbusha sisi na familia na tunapendana hata bila kusema na kuna text ya kwanza haha msiofahamiana ambayo akiisoma tu anajua wewe ni nani,"amesema Chonjo.
Amesisitiza kwamba angependa wote wayafikirie mavazi wanayovaa au mitindo wanayotaka kuichagua kuwa ni text inayotuma ujumbe kwa mabosi wao,wafanyakazi wao,wafanyabiashara wenzao,wapenzi wao,marafiki zao na kwa namna ya kushangaza hata watu wasiowajua au wanaowajua kila siki kwa namna fulani.
Aidha amefafanua Babyshop ni ujumbe unaongea moja kwa moja na watoto ( miaka 0-14), Splash ni ujumbe unaongea moja kwa moja na mabasi,wafanyakazi,wafanyabiashara wenzako kwamba wewe ni mtanashati, Max ni ujumbe rahisi kwa familia kwamba wanaweza kupata kila wakitakacho kwa kila mmoja ndani ya duka moja wakati Shoexpress ni ujumbe rahisi kuyaambia mavazi yako kwamba "hujakamilika bila mimi".
Chonjo amesema wanawaambia wanawataarifu wateja wao ambao wamekuwa wakisafiri umbali mrefu kwenda kwenye maduka yao yaliyoko Mlimani City,GSM Mall Msasani ,Pugu Mall na Aura Mall kuwa wamefungua maduka hayo kwa ajili yao."Sasa tunaweza kufanya kazi na kufanya manunuzi yetu hapahapa katialkati ya Jiji la Dar es Salaam (ndani ya Posta).
"Na kwa kuanza tuna of maalum kwa ajili ya wateja wetu wote wapya na tuliokuwa tayari tunawahudumia kupitia maduka yetu mengine kuanzia Aprili 9 mpaka Aprili 11,2021 ambapo kila ukimaliza manunuzi yako ,ukiwa kaunta,utapasua puto na kujihakikishia punguzo la hadi asilimia 50,"amesema.
Msemaji wa Chapa ya GSM Antonio Nugazi(wa pili kushoto) akitoa ufafanuzi kabla ya kukata keki baada ya kuzinduliwa rasmi kwa maduka mapya ya Kampuni za GSM Group katika jengo la Salamander eneo la Posta Mpya jijini Dar es Salaam, wengine katika picha hiyo ni baadhi ya viongozi wa kampuni hiyo pamoja na wageni waalikwa .Wa kwanza kushoto ni Msanii Omar Nyembo maarufu kwa jina la Ommy Dimpoz ambaye ni balozi wa GSM.Utepe ukikatwa kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa Jengo la Salamander Tower pamoja na maduka mapya ya GSM Group katika eneo la Posta mpya jijini Dar es Salaam.
Ofisa Biashara wa Kampuni ya GSM Group Allan Chonjo akiangalia nguo katika moja ya maduka ya GSM baada ya kuzinduliwa.Maduka hayo yapo katika jengo la Salamander Tower jijini Dar es Salaam.
Mchezaji wa timu ya soka ya Yanga Carlos Carlinhos akichagua fulana baada ya kuingia kwenye maduka ya GSM yaliyopo jengo la Salamander Tower jijini Dar es Salaam.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Shetta (wa kwanza kulia) akiwa na wageni wengine waalikwa akipiga makofi wakati wa ufunguzi wa maduka ya GSM Group yaliyopo jengo la Salamander Tower jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wachezaji wa timu ya soka ya Yanga wakiwa makini kusikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa wakati wa uzinduzi wa maduka ya GSM Group.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment