Shaka Hamdu Shaka ameteuliwa kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi Chama Cha Mapinduzi (CCM) kushika nafasi ya Mtangulizi wake Hamfrey Polepole. Ameteuliwa leo jijini Dodoma mara baada ya Mkutano Mkuu wa Chama hicho Kumchagua Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais Samia Suluhu Hassan.
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)- Ndg Daniel Chongolo (Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya Kinondoni) na Naibu Katibu Mkuu Chama Cha Mapinduzi(CCM)ni Aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Ruvuma, Christina Mdeme.
Katibu wa Itikadi na Uenezi Chama Cha Mapinduzi (CCM), Shaka Hamdu Shaka, ameshika nafasi ya aliyekuwa Katibu mkuu wa chama hicho, Hamfrey Polepole.
Katibu wa Uchumi na Fedha Chama Cha Mapinduzi (CCM), Frank George Hawasi aendelee na nafasi yake, Katibu wa Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC) Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ngebela Lubinga anaendelea na nafasi yake.
Katibu wa Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC) Oganaizesheni, Mama Maurdin Kastiko, ameshika nafasi ya Pereira Silima ambaye atapangiwa kazi nyingine ya kitaifa).
(Ndg Rodrick Mpogolo atapangiwa majukumu mengine ya kitaifa)
Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Juma Sadala Mabodi nae anaendelea na nafasi yake ya awali.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment