Kampuni ya EKARI Moja Tanzania yagawa Miche elfu 45 ARUMERU | Tarimo Blog

Na Woinde Shizza Michuzi Tv
WANANCHI wa vijiji 13 wilayani Arumeru, Mkoani Arusha wameanza kunufaika na mpango wa ugawaji bure wa miche ya kuotesha katika makazi yao itakayowasaidia kuboresha mazingira na kuwaongezea kipato.

Akiongea mapema leo katika zoezi la ugawaji miche 6000 kwa wananchi wa Kijiji Cha Sakila Juu wilayani humo, msimamizi wa miradi ya miti wa kampuni ya Kilimo ya eka Moja Tanzania inayogawa miche hiyo, Esaria Meena alisema kampuni hiyo imejipanga kugawa miche 45,000 kwa vijiji hivyo Katika kipindi cha wiki moja.

Alisema kuwa tangu wazindue mpango huo mwaka 2018 wameshagawa Miche ikiwwmo ya matunda zaidi ya 500,000 na wanampango wa kugawa Miche milioni 5 katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

"Tangu tumeanzisha mpango huu Wananchi wengi wamenufaika kwa kuboresha mazingira,miti ya Matunda, Miche ya mbao ambayo imewasaidia kuongeza kipato na ajira. "Alisema Meena

Alivitaja vijiji vinavyonufaika na mpango huo kuwa ni Njeku, Kikatiti, Maji Moto,Kwa ugoro, Manyire, Maroroni, Migadini, Ngongongare, Muungano, Oldonyongire na Nasholi A na B.

Awali afisa misitu wa halmashauri ya Arusha ,Joseph Masawe ameipongeza kampuni ya Eka Moja Tanzania kwa kuunga mkono sera ya serikali ya upandaji miti ya mwaka 1998 na waraka namba moja ya waziri mkuu inayoitaka kila halmashauri kupanda miti milioni1.5 kila mwaka.

Mwenyekiti wa Kijiji Cha Sakila Juu, Richard Mbise amesema kuwa wananchi wamekuwa na hamasa kubwa ya upandaji wa miti na kuwataka wadau wengine wa mazingira kujitokeza kugawa miti hiyo kwani Katika eneo la ukanda wa Meru linahitaji kupandwa miti ya asili kwa ajili ya mvua na miti ya mikaratusi kwa ajili ya uvunaji wa mbao.

"Mwitikio ni mkubwa sana kwa wananchi wa Sakila Juu hivyo Kuna uhitaji zaidi wa Miche ipatayo 200,000 hivyo tukipata miche hiyo itatosheleza kaya zipatazo 1400. "Alisema

Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Sakila Juu, Emmanuel Mbise na Ekael Palangyo ambao wamenufaika na mpango huo kwa kupata Miche 30 kila mmoja ya aina mbalimbali wamesema kuwa miti hiyo itawanufaisha kwa kuleta mvua na kuvuna mbao na kulitaka kampuni hilo kuendelea kuwapatia miche ya miti ili kuwaongezea kipato.
Mwakilishi wa kampuni ya EKARI Moja Tanzania, Esaria Meena kulia, akimkabidhi miche 30 mwenyekiti wa Kijiji Cha Sakila juu Richard Mbise (kushoto), katika zoezi la ugawaji wa Miche, lililofanyika juzi Wilayani Arumeru katikati ni Afisa misitu wa halmashauri ya Arusha DC,Joseph Masawe(picha na Woinde Shizza, ARUSHA).

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2