Mkurugenzi Kanda ya Afrika Mashariki wa Kampuni ya Utengenezaji wa vipuri vya Magari ya Bosch, Dirk Appelt (kushoto) akimkabiti tuzo ya ushiriano wa kibiashara na Mkurugenzi wa Kampuni ya ya NasTyre Services Limited (NTS), Navin Kanabar wakati wa uzinduzi,uliofanyika Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Uendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Kampuni ya ya NasTyre Services Limited (NTS), Amin Lakhani.
Balozi wa Ujerumani nchini, Regine Hess(wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Kampuni ya NasTyre Services Limited (NTS), Navin Kanabar wakitaka utepe kuzindua ushiriakiano wa kibiashara na utengezaji wa vifaa vya magari ya Kampuni ya Bosch kutoka Ujerumani, Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi wa Kampuni ya NasTyre Services Limited (NTS), Navin Kanabar akizungumza baada ya kuzindua ushiriano wa kibiashara na Kampuni ya utengezaji wa vipuri bora vya magari ya kutoka nchini Ujerumani ya Bosch, uliofanyika Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha watoa Huduma za Makampuni za Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS), Abdulsamad Abdulrahim wakati wa uzinduzi wa ushirikiano wa Kibiashara na makampuni za NasTyre Services Limited (NTS) na Bosch zinazotengeneza wa vipuri vya kisasa vya magari vya kisasa.
Balozi wa Ujerumani nchini, Regine Hess wapili kulia (wa akiangalia mashine za kisasa za utengenezaji wa vipuri vya magari ya Kampuni ya NasTyre Services Limited (NTS) baada ya kuzindua ushiriakiano wa kibiashara na utengezaji wa vifaa vya magari ya Kampuni ya Bosch kutoka Ujerumani, Dar es Salaam.
KAMPUNI ya magari ya Tanzania NasTyre Services Limited (NTS) kwa kushirikiana na kampuni ya Kijerumani ya Bosch zinatarajia kukuza wigo kwenye huduma za usafirishaji kwa kutoa ajira kwa vijana zaidi ya 100 wa kitanzania ili kukuza sekta ya viwanda na usafirishaji.
Hatua hiyo imekuja kufuatia Kampuni hizo mbili, NTS na BOSCH za utengenezaji wa vipuri vya magari kuungana na kuzipa nguvu katika kutoa huduma kwa watanzania zitakazokuwa bora na kwa bei nafuu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Muunganiko wa kampuni hizo mbili, balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Regine Hess amesema, Muunganiko wa makampuni hayo mawili utaongeza ajira na kukuza sekta ya viwanda nchini.
"Nawapongeza Nas Tyres hasa kwa utayari wao kushirikiana na kampuni yenye sifa kimataifa ya Bosch kwani kupitia ushirika huu sekta ya huduma za magari itaboreka zaidi." amesema balozi Hees.
Kampuni ya NasTyre Services Limited (NTS), ni kampuni ya magari ya Tanzania na moja ya waagizaji wakubwa na wasambazaji wa matairi na betri imeongeza huduma zake kupitia ushirika wa kibiashara ilioingia na Bosch, ambayo ni kampuni mashuhuri ya magari ya Ujerumani ambayo inafanya kazi sehemu mbalimbali duniani.
Amesema, ushirikiano mpya huo utafanikisha kutawala soko katika sekta ya utoaji huduma za magari nchini Tanzania. Kutokana na ushirikiano huu, NTS inakuwa kituo kinachowezesha mteja kupata huduma zote za magari yao katika sehemu moja.
Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa NTS, Amin Lakhani amesema, "tunajivunia kwa kuuza bidhaa bora zenye viwango vya kimataifa sambamba na huduma bora, kwa kipindi cha miaka 10 sasa Watanzania wamekuwa wakinufaika na uwekezaji wetu katika sekta hii, kwa sababu hiyo, tumeona ili kukuza zaidi huduma zetu tutumie fursa hii kushirikiana na Bosch kibiashara ili kuendelea kuwapa wateja wetu huduma bora zaidi na kwa gharama nafuu." Amesema.
"Pamoja na kuongezwa kwa huduma za Bosch katika huduma zetu, mafundi magari wa Tanzania na vijana kwa jumla watapata fursa za mafunzo pamoja na mafunzo maalum nje ya nchi ili kukuza ujuzi wao kwa maneno mengine, kupitia ushirika huu, NTS inafungua milango ya fursa kwa vijana wa kitanzania katika sekta hii." Amebainisha Lakhani
Akizungumzia ushirikiano wake na NTS, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Bosch Manoj Thakkar amesema NTS ina uhusiano mzuri katika tasnia ya magari na inajulikana kwa ubora wake, huduma za hali ya juu. "kwa hivyo kutoka kwa mtazamo wa biashara, ushirikiano huu utanufaisha pande zote mbili."
Naye Abdulsamad Abdulrahim, Mwenyekiti wa watoa huduma katika sekta za mafuta na gesi Tanzania ATOGS amesema kuwa kutokana na cha serikali iliyopo madarakani hivi sasa kutoa kipaumbele kwa wawekezaji, anaamini kufuatia uwekezaji huo nchi itaendelea kupiga hatua kutoka kwenye uwekezaji mdogo kwenda mkubwa jambo litakalosaidia kuendeleza kukuza uchumi wa nchi.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment