KATIBU MKUU UJENZI AKABIDHIWA OFISI | Tarimo Blog

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga (kulia) akikabidhi nyaraka za makabidhiano ya ofisi kwa Katibu Mkuu mpya wa Sekta hiyo, Mhandisi Joseph Malongo, katika Ofisi za Wizara hiyo zilizopo Mtumba jijini Dodoma.

Katibu Mkuu  wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Malongo , akitoa maelekezo kwa  wajumbe wa Menejimenti ya Sekta ya Ujenzi mara baada ya kukabidhiwa  Ofisi na aliyekuwa  Katibu Mkuu wa  Sekta ya hiyo, Arch. Elius Mwakalinga (Kulia), kwenye Ofisi za Wizara hiyo, zilizopo Mtumba jijini Dodoma.

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga (kulia), akimuonesha baadhi ya nyaraka Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Malongo, wakati akimkabidhi ofisi, Mtumba jijini Dodoma.

Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (hayupo pichani), wakati akitoa maelekezo katika kikao cha kukabidhiwa Ofisi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Sekta hiyo, Mtumba jijini Dodoma.

PICHA NA WUU


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2