Kiwanda cha magari mapya– GF vehicles Assemblers chatengeneza Magari 100 kwa miezi mine ya kwanza | Tarimo Blog

Kiwanda kipya cha kutengeneza na kuunganisha Magari nchini Tanzania GF vehicles Assemblers (GFA) kilichopo Kibaha mkoani Pwani leo kimetimiza utengenezaji wa Gari ya miamoja (100)  kuanzia kipindi cha mwezi Januari hadi Aprili.

Akizungumza wakati wa sherehe za kuruhusu gari ya 100 kukanyaga aridhini baada ya kuunganishwa tayari kwa kutembea ,Meneja mkuu wa kiwanda hicho ,Ezra Mereng alisema ni kazi ngumu kukamilisha zoezi la uunganishaji na utengenezaji wa magari hayo kwa kuwa Tanzania sisi ndio Kiwanda cha kwanza kutengeneza (kuunganisha) magari .

Changamoto ni nyingi kutokana na kutokuwa na wataalamu wengi katika sekta hii ya Magari, lakini kwa kushirikiana na wataalamu wa nje tuliweza kuunganisha magari 10 ya awali na baadae wao wakaondoka na tukabaki na watanzani wenzetu ambao kwa uwezo wa Mungu leo tumefanikiwa kumaliza gari ya 100.

Pia alizitaka Tasisisi za serikali na kuagiza magari ambayo hayajaunganishwa na kazi ya kuunganisha ifanyike na viwanda vya ndani ili kukuza pato la taifa na kuongeza ajira kwa watanzania, pia kama nchi itajipatia fedha za kikgeni kwa kuuza nchi jirani Magari yanayotoka Tanzania.

Nae afisa masoko na manunuzai wa kampuni ya uuzaji wa magari ya FG Trucks & Equipments Ltd , Hamis Hasasn ambao ni moja ya wateja waliopeleka kazi ya kuunganishiwa Magari yao katika kiwanda hicho alisema,Mwanzo wateja walikuwa hawaamini kama magari hayo yatakuwa na ubora sawa lakini kwa kipindi hiki magari yapo mitaani na yanafanya vizuri,alisema Hamis na kuongeza kuwa kiwanda hicho kimeajiri Wafanyakazi 100  wenye ajira za kudumu, mikataba pamoja na za muda mfupi .

Meneja mkuu wa kiwanda cha kutengeneza Magari mapya cha Kwanza nchini Tanzania GF- Vehicle Assembly Ltd , Ezra Mareng akizungumza na wateja wa kiwanda hicho kilichopo Kibaha mkoani Pwan wakati wa sherehe ya kutimiza Magari 100 yaliotengenezwa na kiwanda hicho kwa kipindi Cha miezi Minne.



 


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2