Kwa nini hakuna kidonge cha kudhibiti uzazi kwa wanaume? | Tarimo Blog

Je,Wanaume watakubali kutumia vidonge au njia za kupanga uzazi?
CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Hadi sasa hakuna kidonge cha kupanga uzazi kwa wanaume , licha ya juhudi nyingi za hapo awali kukitengeza.

Utengezaji wa kidonge cha kupanga uzazi kilibadilisha ulimwengu wakati kilipoletwa katika jamii mnamo miaka ya 1960.

Hivi sasa, vidonge hivi hutumiwa na wanawake wapatao milioni 214 ulimwenguni kote na wana soko la kila mwaka karibu la Dola za Marekani milioni 18,000.

Hata hivyo, ingawa zaidi ya miongo sita imepita tangu "uwasilishaji rasmi" wa kidonge, kati ya orodha ya njia 20 za kupanga uzazi ambazo Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) inazo, ni mbili tu zinazoweza kutumiwa na wanaume.

Kwa nini hakuna kidonge cha kudhibiti uzazi kwa wanaume ?

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

"Wazo la kutengeza mpango wa uzazi kwa wanaume limekuwepo karibu kwa muda mrefu kama utengezaji wa mbinu ya upangaji uzazi kwa wanawake." Adam Watkins, profesa wa biolojia ya uzazi katika Chuo Kikuu cha Nottinghan, aliiambia BBC World.

Kulingana na Watkins, changamoto kuu ya matibabu imekuwa kwamba, wakati mwanamke anatoa yai moja kwa mwezi, mwanaume hutoa mamilioni ya mbegu kila siku.

Hiyo ndiyo changamoto, kwamba hata kama mwanamume atapoteza 90% ya uwezo wake wa kuzalisha manii, bado ana rutuba, anasema mtaalam huyo.

Ingawa hii sio sababu kuu kwa nini kidonge chenye ufanisi na salama hakijatengenezwa.

"Nadhani ikiwa haijatengenezwa vyema imekuwa kwa sababu ya mafanikio ya kidonge cha upangaji uzazi kwa wanawake.

Inafanya kazi vizuri na ni bora sana kwamba, kwa mtazamo wa kiuchumi, kampuni nyingi za dawa hazihisi kuwekeza katika kidonge cha wanaume'

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mbinu mbili za upangaji uzazi kwa wanaume kwenye orodha ya WHO ni kondomu na vasektomi.

Kwa mtaalam, hii imesababisha kampuni za dawa kutowekeza katika utafiti na maendeleo ya miradi ambayo inasababisha mfano wa kidonge salama cha kupanga uzazi kwa wanaume .

"Kwa sababu tofauti, mzigo wa upangaji uzazi ulitwika wanawake .

Wao ndio wamekuwa wakiwajibikia jukumu hilo pekee yao hatua ambayo sio sawa'ameongeza msomi huyo.

Habari hii iliandaliwa na BBC.COM Aprili 5, 2021

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2