MSIWAUE WADUDU WACHAFUSHAJI: DKT KAMATULA | Tarimo Blog

 


 

Na Sixmund J. Begashe

Jamii imetakiwa kuwatunza wadudu wachavushao kwa sababu ni muhimu kwa maisha ya binadamu na uzalisaji wa mazao mbalimbali, hivyo jamii inatakiwa isiwaue ili waendelee kutunufaisha

Wito huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa, Dkt. Gwakisa Kamatula katika uzinduzi wa onesho Maalumu la Wadudu Wachavushaji lilowekwa na Wahifadhi wa Baolojia wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam kwa kushirikiana na wadau mbali mbali.

Wataalamu wetu wa hapa Mkaumbusho ya Taifa wamekuwa na utaratibu wa kufanya utafiti wa kibaolojia na kuhakikisha matokeo ya tafiti hizo zinahifadhiwa, kwa matumizi ya kimakumbusho na pia kuelimisha jamii kupitia maonesho na makongamano mbali mbali, hivyo nitoe wito kwa watanzania wote kuitumia Taasisi yetu kujifunza mambo mbali mbali ya Kibaolojia hasa umuhimu wa hawa wadudu wanaochavusha.” Aliongeza Dkt Kamatula.

Akizungumzia maonesho hayo, Mhifadhi Mwandamizi wa Baolojia ambaye pia ni Mratibu wa tukio hilo Bi Adelaide Salema amesema, maonesho hayo yamehusisha, wadau mbali mbali wanao jishughulisha na uhifadhi wa mazingira, maonesho ya Picha, Video, bustani ya vipepeo pamoja na mkutano wa wanasayansi wa Baolojia nchini.

Lengo letu kubwa ni kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule za sekundari na msingi ambao tunaamini ndio warithi wazuri ambao watakuja kuwarithisha vizuri watoto wao juu ya umuhimu wa wadudu wanaochavusha, lakini pia kupitia mkutano wa wataalam tunaweza kubadilishana uzoefu wa namna ya kuhifadhi na kushirikishana matokea ya tafiti zetu kupitia Tehama.” Alisema Bi Adelaide Salema

Mhadhiri Mwandamizi kutoka Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Dkt Finian Mwalongo  ambaye pia ni msimamizi mkuu wa kikosi kazi cha utengenezaji wa Mfumo ujulinao kwa jina la TanBIF PORTAL, katika mkutano huo wa wadau ameeleza upo umuhimu wa wanasayansi nchini kutumia mfumo huo ili kuongeza tija katika tafiti mbali mbali za kisayansi.

Mfumo huu ni muhimu sana kwa wanasayansi nchini maana unawawezesha kukusanya taarifa za baionuai kutoka sehemu mbali mbali, pia data za viumbe kama wadudu ambao wanafaida kubwa kiuchumi kama vile kilimo na kiutali kisha kuzichakata na kutoa fursa zitumike na watafiti wengine ili kuchochea tafiti zaidi” Alisisitiza Dkt Mwilongo

Bw Robart Muhangwa ambaye ni mmiliki wa Bustani ya Prince (Prince Garden), ameipongeza makumbusho ya Taifa kwa kuandaa maonesho hayo na kumshirikisha kwani imekuwa ni furusa kubwa kwake ya kujifunza na kutoa elimu kwa jamii namna ya kutengeneza bustani ambazo ni rafiki kwa mazingira na uhai wa wadudu wanaochafusha.

Nae Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge, Moses Efrahimu na wa Shule ya Sekondari Magomeni Asha Juma, wameomba jamii kuacha kuwauwa wadudu wachafushaji kama vile Vipepeo, Nyuki, Nondo na wengineo kwani wanafaida kubwa kwenye maisha ya jamii hasa katika kuhakikisha upatikanaji wa chakula cha kutosha.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2