Kwa jinsi ninavyoona mwelekeo wa serikali ya Mheshimiwa. Mama Samia Suluhu Hassan ni wazi anataka kufanya mabadiliko ya kiuchumi, sasa tumsaidie ili tuwezekuwa na diplomasia ya uchumi wa kweli na biashara sio siasa na uongozi .
Maana Mheshimiwa Samia ameanza na Wizara mbalimbali, kaja makatibu wakuu na wakuu wa tasisi za serikali, pia atateua wakuu wa mkoa, wilaya na wakurugenzi wa mkoa(DED) Wakurugenzi wa Wilaya (DES).Huenda akaanzana wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama au mabalozi wanaowakilisha nchi yetu.
Si vibaya kutoa ushauri kwenye hizi balozi zetu. Hasa kipindi hichi anafanya uteuzi na marekebisho makubwa kwa ajili ya uchumi wetu.
Na sivibaya kuiiga baadhi ya nchi zilizofanya diplomasia ya uchumi wa kweli mfano India, USA, China nk. Hizi nchi zote huwa inatumia raia wao ambao ni wataalamu (experts) wanaoishi kwenye nchi husika.
Mfano Balozi ya China, huwatumia raia wake waliopo kwenye nchi husika kushauri juu ya biashara na uwekezaji na kigezo kikubwa wanachokitumia ni ufahamu wa lugha ya nchi husika, utamaduni na desturi zao.
Ni muda sasa wakutumia waTanzania wenzetu wanaoishi nje ya nchi walioondoka nchini kihalali na ishi kihalali ughaibuni na ni wataalam ( experts) na wana elimu ya kutosha na hawana kashfa ya aina yoyote pia wawe wanaifahamu vema lugha pamoja na desturi na utamaduni ya nchi husika.
Mfano unamtoaje mtu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na kumpeleka nchi kama za Falme za kiaarabu, Urusi, China, S.Korea ambao kingereza sio lugha yao na Afisa mteule hajui lugha ya pale ( local language) wala utamaduni ya nchi husika? Na anaenda kufanya kazi kama Mwambata wa Elimu ( Education Attache) au mwambata wa biashara( Commercial Attache) huku ni kupoteza rasilimali fedha kwa sababu hataweza kufanya kazi kifasaha maana atahitaji sio chini ya miaka miwili kujua lugha husika na utamaduni zao.
Kwanini tusichukue waTanzania wenye vigezo ambao wapo nchi husika ili kupunguza gharama za kuleta mtu toka wizarani ambaye atakuja kusimamia elimu wakati hajui system ya nchi hiyo au aje kusimamia kitengo cha biashara wakati hawezi kuwasiliana na wawekezaji wakubwa kwa lugha yao? Sana sana atapatikana mtu wa kati na mawasiliano ya one on one direct yanakuwa hayapo.
Mfano kwa China kwanini Serikali isimtumie mtu kama Dkt Lyatamila (PhD), ningeshauri huyu dada apewe nafasi either ya Mwambata wa Elimu au (Education attaché) Mwambata wa Biashara (commercial attaché) kwa sababu sehemu zote mbili ana fit kwanza ni Senior Lecturer wa Chuo Kikuu hapa China kwa maana yupo ndani ya system ya Elimu ya China pili ni mtalam wa masoko kwa maana ni PhD wa Marketing management na ameishi China zaidi ya miaka 15, anaifahamu vizuri lugha yao, utamaduni wao na desturi zao.
Kwahiyo atafaa kwenye majadiliano ya pande zote mbili either kujadili kusaidia na kusimamia wanafunzi kwa niaba ya Serikali , haswa ukizingatia wanafunzi wengi wanakuja nchi hii kwaajili ya kusoma au mijadala ya wawekezaji na wafanya biashara kwakuwa anajua kuongea, kusoma na kuandika kwa lugha yao, ingawa ni mwalimu anayefundisha kwa lugha ya kingereza . By the way Degree yake ya kwanza ni ya sheria amesomea hapa hapa Tanzania then akafanya Masters na PhD Business Administration in Marketing.
Kwa kufwatilia kwangu nimegundua kwamba huyu dada amefwata taratibu za nchi zote mbili mpaka kupata kazi na sheria ya China ili kuajiriwa kama mtalaam ( expert) ni lazima uwe na post-doctorate na mikataba utagongwa mihuri na kusaidiwa na wizara ya nje na ubalozi wa China uliopo nchini kwako .
Msinielewe vibaya simaanishi hamna waTanzania wengine wasiofanya kazi nchini China ila huyu Dkt Lyatamila ndiye anayetambulika na Serikali zote mbili wengine wanatambulika na mashirika au ofisi zao tu.
Namalizia nchi yetu bado ni ndogo kiuchumi ni vizuri kutumia rasilimali watu kwenye balozi zetu wanaoishi nje ya nchi haswa kwenye post ndogondogo , hii itasaidia kuokoa fedha.
Dkt Lyatamila ni mfano tu lakini wapo waTanzania wengi kila nchi wenye vigezo kama vyake au zaidi .
HII NDO DHANA YA KIDIPLOMASIA , KUTUMIA KIDOGO KUINGIZA KINGI
Nawasilisha ,
Mimi Dr. Salma Ahmed Fakhi
Mwanafunzi Mwaka wa Pili
Beijing-China
Email: 2323427659@qq.com
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment