Mbunge wa Mbeya Mjini ambaye ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Mbeya, Dkt. Tulia Ackson akishirikiana na wabunge kutoka Mbeya na Songwe kuzindua Umoja wa Watu wa Mbeya na Songwe wanaoishi Dodoma (UWAMBESO) jijini Dodoma. Umoja huo ambao umesajiliwa rasmi Oktoba 2021 una wanachama 142.
Kutoka kushoto ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Songwe, Neema Mwandabila, Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga, Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi na kutoka kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Wazazi, Bahati Ndingo, Katibu Mkuu wa Uwambeso, Baleke Moses na Mwenyekiti wa umoja huo, Nsubi Bukuku.
Wabunge kutoka mikoa hiyo wamehidi kuchangia sh. mil. 9 kutunisha mfuko wa Uwambeso pamoja na kujiunga uwanachama.
Katika hafla hiyo uongozi uliwakabidhi vyeti waasisi na na viongozi waanzishilishi wa umoja huo ikiwa ni shukrani ya kutambua mchango wao uliofanikisha uwepo wa umoja huo muhimu.
Dkt. Tulia licha ya kuwapongeza kuanzisha umoja huo ameutaka uongozi ktanua wigo wa umoja huo kwa kuanzisha matawi katika wilaya zote za mkoa wa Dodoma pamoja na kuanzisha Uwambeso katika mikoa mingine nchini. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mwenyekiti wa Uwambeso, Nsubi Bukuku akimkabidhi cheti Mbunge wa Mbeya Mjini na Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson ikiwa ni shukrani ya kutambua mchango wake katika umoja huo.Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanznania, Dkt. Tulia Ackson (katikati) wabunge na viongozi wa Uwambeso wakikata keki wakati wa uzinduzi wa umoja huo wa watu kutoka mikoa ya Mbeya na Songwe wanaioshi Dodoma.
Dkt. Tulia akimlisha keki Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya ambaye ni Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi.
Mbunge wa Viti Maalumu, Wazazi Taifa, Bahati Ndingo (kushoto) akifurahia na wajumbe baada ya kukabidhiwa keki iliyonunuliwa na wabunge kutoka Mkoa wa Mbeya.
Dkt. Tulia akihutubia na kuwaambia wajumbe kuwa amefrahishwa na uanzishwaji wa umoja huo na kwamba wabunge wote kutoka mikoa hiyo wako tayari kujiunga. Pia wabunge hao waliahidi kuuchangia umoja huo sh. mil. 9. Dkt. Tulia akimlisha keki Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga.
Mbunge wa Viti M aalumu (CCM Wazazi Tanzania Bara), Bahati Ndingo kutoka Mkoa wa Mbeya akilishwa keki na Dkt. Tulia.
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Songwe, Neema Mwandabila akilishwa keki Mmoja wa wanachama wa Uwambeso akilishwa keki kwa kuchangia fedha za kutunisha mfuko wa umoja huo.
Ni furaha iliyoje wakati wa hafla hiyo
Wanachama wa Uwambeso wakigongeana glasi na viongozi walio meza kuu kwa kutakiana heri
Wanachama wa Uwambeso wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi Dkt Tulia.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment