MKUTANO Mkuu Maalum wa Chama cha Mapinduzi CCM ulioketi leo jijini Dodoma umempitisha Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mwenyekiti wa Sita wa chama hicho akipata kura za ndiyo kwa asilimia 100.
Rais Samia amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho na Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli kilichotokea Machi 17 mwaka huu.
Akitangaza matokeo hayo, Mwenyekiti wa uchaguzi huo ambaye pia ni Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema kura zilizopigwa ni 1,862 ambapo kura za Ndiyo zilikua zote 1,862 ikiwa ni Asilimia 100 ya kura zote.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment