Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mvomero,kuhakikisha shule ya Msingi shikizi ya Sokoine inapata Walimu wa kuajiliwa na Serikali, kwani kwa sasa Shule hiyo haina Walimu ambao wanasifa na vigezo vya kufundisha Wanafunzi.
Mkuu wa Mkoa ametoa agizo hilo mbele ya Wananchi katika mkutano wa Hadhara wenye lengo la kutatua mgogoro Ardhi kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro na Wilaya ya Mvomero, uliodumu ndani ya miaka tisa,wakigombania mpaka wa Kijiji cha Mkono wa mara,ambapo kila upande ukidai Kijiji hicho kipo katika Wilaya yake.
Akizungumza mala baada ya kutatua mgogoro huo Mkuu wa Mkoa Ole Sanare,akaitaka Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero kukamilisha ujenzi wa madarasa kwenye shule ya Msingi Shikizi ya Sokoine ambayo ainachumba kimoja cha madarasa,huku ikiwa na wanafunzi zaidi ya mia tatu walio katika mikondo tofauti.
Aidha akizungumzia mgogoro huo Mkuu wa amkoa wa Morogoro amesema mgogoro huo umedumu kwa kipindi kirefu lakini ofisi yake kwa kushirikiana na ofisi ya ardhi tayari wamemaliza mgogoro huo.
Katika hatua nyingine Ole Sanare amewataka viongozi wa Vijiji kuacha tabia ya kuuza maeeneo pasipo kufuata sheria na taratibu jambo ambalo linasababisha migogoro ya Ardhi ya katika maeneo mengi Mkoani Morogoro.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa kaenda mbali zaidi na kuwataja baadi ya viongozi wakiwemo wa chama cha Mapinduzi CCM wanaotuhumiwa kuuza maeneo pasipo kufuata sharia katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomoro akiwemo Mzee Kinyau na Mzee Koka,huku akiagiza kufanywa uhakiki kwa wale wote wanaomiliki maeneo katika Halmashauri hiyo.
Kwa upande wake Kamishina wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Morogoro Frank Minnzikuntwe amesema baada ya kupokea maagizo ya kutoka kwa Mkuu wa Mkoa aliunda tume iliyohusisha pande zote mbili za Wilaya ya Mvomero na Morogoro na kumaliza kabisa mgogoro huo.
Nao baadhi ya wananchi wasema kutatuliwa kwa mgogoro huo utachochea maendeleo kwani walikosa namna ya kutatua kero zao kwai walikua hawajua wapo upande gani.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment