MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya kuwepo kwa upepo mkali na mawimbi makubwa katika maeneo ya pwani ya Tanzania kwa siku mbili, Aprili 22 na 23, 2021.
Maeneo yanayotarajiwa kuathirika ni Pwani ya Bahari ya Hindi katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Dar es Salaam, Tanga, visiwa Mafia pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba
Mamlaka hiyo, kupitia taarifa yake ya leo Alhamisi Aprili 21, 2021 imesema kunatarajiwa kuwepo na upepo mkali wa kasi ya kilomita 40 kwa saa na mawimbi yanayofikia mita 2.
Mamlaka imesema, uwezekano wa kutokea ni wastani na kiwango cha athari kinachoweza kutokea ni wastani huku athari zinazoweza kujitokeza ni kuathirika kwa baadhi ya shughuli za uvuvi na usafirishaji.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment