TAWA WASAINI HATI YA MAKUBALIANO NA WCS | Tarimo Blog

Na Farida Saidy, Morogoro
MAMLAKA ya usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) na shirika lisilo la Kiserikali la Uhifadhi wa Wanyamapori Wildlife Conservation Society (WCS0 wamesaini hati ya makubaliano ya yenye lengo la kuhakikisha kunakuwa na ushirikiano katika kuanzisha miradi mbalimbali katika mfumo wa ikolojia ya Ruaha na Katavi inajumisha Mapori ya  Rungwa, Muhesi, Kizigo, Lukwati, Piti na Rukwa Kwafi.

Akizungumza mala baada ya utiaji saini huo Kaimu Kamishna wa Uhifadhi  Mabula Misungwi Nyanda amesema utijia saini huo unamaana kubwa sana katika Uhifadhi wa Wanyamapori na mapambano dhidi ya Ujangili katika katika Mapori yalio chini ya TAWA.

Aidha Misungwi ameishukuru WCS kwa juhudi wanazofanya katika Uhifadhi na mashirikiano yao na TAWA katika kuhifadhi rasilimali zilizopo katika maeneo wanayoyasimamia,huku akiongeza kuwa Ujangili ni swala mtambuka na linahitaji kuunganisha nguvu za pamoja,hivyo amewaomba WCS wasichoke katika juhudi za kupambana na majangili.

Nae Mkurugenzi wa WCS Tanzania, Noah Mpunga aliwashukuru TAWA kwa ushirikiano wao wanaoesha katika mapambano dhidi ya ujangili na kusisitiza kuwa ni muhimu kushirikiana kwa pamoja ili TAWA waweze kufikia malengo yao.

Katika hafla ya hiyo ya makabidhiano iliyofanyika katika Ofisi za Mkao Mkuu ya TAWA Mkoani Morogoro, TAWA iliwakilishwa na Kaimu Kamishna wa Uhifadhi Bwana Mabula Misingwi Nyanda huku WCS ikiwakilishwa na Mkurugenzi wa WCS Tanzania Bwana Noah Mpunga.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2