Kaimu Mkurugenzi wa Biashara wa TTCL Laibu Leonard (kushoto,) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na urejeshaji wa vifurushi vya data, dakika na SMS uliyofanywa na shirika hilo ambapo amesema TTCL itahudumia wateja na watanzania wote kwa weledi na ubunifu ili kukidhi mahitaji ya wateja wao, Leo jijjni Dar es Salaam.
Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
SHIRIKA La Mawasiliano Tanzania (TTCL,) limesema litaendeleza azma yake ya kutoa mawasiliano kwa watanzania kwa kutoa vifurushi vya bei nafuu na kuwataka watanzania kurejea nyumbani kwa kuwa huduma zimenoga na hiyo ni pamoja na huduma nyinginezo zikiwemo huduma za fedha ambazo hutolewa kwa weledi, ubunifu na zenye kukidhi mahitaji ya wateja na watanzania kwa ujumla.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Kaimu Mkurugenzi wa biashara wa TTCL Laibu Leonard amesema, baada ya Shirika hilo kutoa bei mpya ya vifurushi vya intaneti, dakika na jumbe fupi yaani SMS na wananchi ktoa maoni yao serikali ilisitisha gharama mpya za vifurushi na kuagiza watoa huduma za mawasiliano kurejesha huduma za vifurushi vya zamani na TTCL ilikuwa shirika la kwanza kufanya hivyo.
Leonard amesema, shirika hilo lilikuwa la kwanza kutii agizo za serikali na Aprili 3 walirejesha huduma za vifurushi kwa gharama za awali na kutoa fursa kwa wateja wao kupata huduma bora za mawasiliano zenye kukidhi mahitaji yao.
"TTCL tunapenda kuwataarifu wateja wetu na watanzania kwa ujumla kuwa vifurushi vyetu vya zamani vyenye gharama nafuu vimerejea kama kawaida, hivyo tunawaalika watanzania waendelee kufurahia huduma zetu na wateja wetu wanaweza kupata huduma za vifurushi vyetu kwa kupiga *148* 30# na huduma za kifedha (T-PESA,) kupitia *150*71# na kufurahia huduma zetu zenye uhakika na gharama nafuu." Amesema.
Aidha ametumia wasaa huo kuwakaribisha watanzania ambao hawajarudi nyumbani kutembelea wakala wao waliosambaa maeneo mbalimbali nchini pamoja na vituo vya huduma kwa wateja ili waweze kusajili laini zao pamoja na kupata huduma nyingine za mawasiliano.
Amesema kuwa, TTCL inakwenda na wakati na ni wasaa wa watanzania kulinganisha bei kwa kutembelea TTCL kujisajili na kupata huduma mbalimbali zikiwemo zile zisizo na ukomo na kuzifurahia na kueleza kuwa shirika hilo litaendelea kuhakikisha wanatoa huduma za mawasiliano kwa weledi na ubunifu wenye kukidhi mahitaji ya wateja wao na watanzania kwa ujumla.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment