Na Woinde Shizza, Michuzi TV- ARUSHA
VIJANA wametakiwa kuilinda amani iliyopo kwa kushiriki katika uhifadhi wa rasilimali zilizopo nchini pamoja na kuhamasisha utalii wa ndani ili uchumi wa nchi uendelee kukuwa kwa kasi .
Hayo yamesemwa na kamishna mwandamizi wa shirika la hifadhi za taifa (TANAPA) kanda ya kaskazini Herman Batho akizungumza katika kongamano la vijana lenye lengo la kueleza umuhimu wa vijana katika kuendeleza shughuli za utalii lililofanyika jijini Arusha.
Alisema kwa kuwa vijana ni nguvu kazi kubwa ya taifa wanapaswa kuilinda amani iliyopo kwa kulinda rasilimali zilizopo nchini na kuhamasisha utalii wa ndani ili pato la nchi liendelee kukuwa zaidi kutokana na uwepo wa watalii wengi wanaotembelea hifadhi.
Alisema ni vyema kila mtanzania akajua na kujiuliza ni kwa namna gani anaweza kuchangia kuendeleza sekta ya utalii haswa katika kipindi hiki ambacho wageni wanaotoka nje ya nchi kuja hapa nchini wamepungua kutokana na nchi zao kufugwa (lockdown) uliyosababishwa na uwepo wa ugonjwa wa Covid 19.
“tunatakiwa watanzania tuinuke tusilale tu kisa watalii kutoka nje hawaji kutembelea mbuga zetu basi na sisi tusiende kutembelea, tunatakiwa tuamke sisi kama sisi tutembelee tuhamasishane kutembelea hifadhi zilizopo hapa nchini ukizingatia gharama zake kwa sisi wazawa ni ndogo sana ambazo mtanzania yeyote yule anaweza kuzimudu,watanzania tupo zaidi ya milioni 60 kulingana na sensa iliyofanywa hapo awali lakini ukiangalia ni wangapi wanaotembelea hifadhi zetu kwa kipindi kwa mwaka uliopita ni watanzania milioni moja laki tano tu ndio wametembelea jambo ambalo halirizishi kabisa “alibainisha Batho.
Kwa upande wake mwenyekiti wa bunge la vijana wa jumuiya ya afrika mashariki Jemsi Leonadi alisema kuwa wao kama vijana wamejipanga kuwahamasisha wananchi wote kutembelea hifadhi zetu ili pato la nchi liendelee kukuwa na uchumi uendelee kupanda zaidi .
Alisema kuwa tunapokuwa na rasilimali kikubwa zaidi kinachotakiwa ni kujitangaza zaidi na kuhamasisha zaidi utalii wetu kwani tunapohamasisha utalii wetu wa ndani inasaidia hata vijana ambao hawana ajira kupata ajira kwani pindi wageni wanavyokuja au watu wanavyotembelea hifadhi zetu ndivyo jinsi ajira zinaongezeka.
Aliwataka wananchi hususa ni vijana kuendelea kulinda rasilimali tulizoachiwa na waasisi wa nchi zikiwemo mbuga za wanyama, wanyama wenyewe waliopo katika hifadhi zetu,milima, mapori yetu ya akiba, maziwa yetu pamoja na madini ambayo tunayo ili yaje yavisaidie vizazi vyetu vya baadae.
Aidha aliwasisitiza wananchi kuendelea kuilinda amani ambayo tuliyonayo bila kuvurugwa na mtu yeyote kwani tunapoipoteza amani hii hatutaweza kufaidi vitu vizuri ambavyo tunavyo na tulivyobarikiwa na Mungu kuwa navyo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment