Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Valentino Hongoli akiwaagiza watendaji wa kata za halmashauri hiyo kuzingatia taratibu za manunuzi ili kuepuka kuingia katika migogoro na halmashauri hiyo na kupelekea kufukuzwa kazi.
Na Amiri Kilagalila,Njombe
WAFABIASHARA wamewatuhumu na kufikisha malalamiko yao kwa uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe dhidi ya baadhi ya watendaji wa halmashauri hiyo kuwaomba kupandisha ghalama za vifaa wakati serikali inapohitaji kununua vifaa vya ujenzi wa miradi ya maendeleo ili waweze kugawana sehemu ya manunuzi.
Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Valentino Hongoli wakati wa kikao cha baraza la madiwani cha kupokeana kujadili taarifa za kata kilichaofanyika katika kata ya Mtwango wilayani humo.
“Kuna baadhi ya wafanyabiashara wanatoa mashtaka kuwa kuna watendaji wasio waaminifu wanawashawishi wafanyabishara kupanga bei kubwa kwenye vifaa ili na wao wapate asilimia,tunaendelea kufuatilia kwasababu kuna wafanyabiashara mnaoenda kununua vifaa huko baadhi yao wana ndugu huku kwa hiyo wanapata uchungu”Valentino Hongoli aliwaeleza watendaji mbele ya baraza la madiwani.
Mwenyekiti amewaagiza watendaji kuacha tabia hiyo kwa kuwa taarifa hizo zimeifikia halmashauri na inaendelea kuwafuatilia.
“Hao watendaji niwaagize waache mara moja kwasababu taarifa zao tunazo na tunaendelea kuwafuatilia hatua kwa hatua na tutakapokukamata ujue kazi huna”alisema Hongoli
Hongoli amewaomba watendaji wa kata kuzingatia swala la manunuzi kwa mujibu wa sheria na maelekezo ya serikali.
“Samba mba na hilo kwenye ufundi maelekezo yako wazi kwamba tunapotafuta mafundi tunatakiwa tuwe tunashindanisha ili kumpata fundi anayeweza kutekeleza mradi vizuri na kwa bei naafu,kwasababu kama halmashauri tunategemea kutofautiana kwenye usafirishaji wa vifaa vya ujenzi lakini kwenye bei za manunuzi tungeweza kuwiana na ukizngatia baadhi ya miradi tunayoletewa na serikali ina ramani moja”alisema Hongoli
Baadhi ya watendaji akiwemo Majula Mjungu mtendaji wa kata ya Matembwe na Faustine Katende mtendaji wa kata ya Ikondo wamekiri kupokea maelekezo ya mwenyekiti wa halmashauri hiyo na kwamba huenda kweli wakawepo watendaji wanaokosa maadili na kukiuka kanuni za manunuzi.
“Sisi tupo wengi na inawezekana wapo wanaofanya hivyo niombe waache tu wale wanaofanya hivyo kwasababu ni kinyume na utaratibu wa utumishi wa uma na kama kifaa inabidi ununue kaulingana na bei ilivyo ili pesa unayopata uweze kufanya kazi sehemu kubwa”alisema Majula Mjungu
Hata hivyo mwenyekiti wa halmashauri hiyo ameishukuru halmashauri katika ukusanyaji mzuri wa mapato uliosadia kufanikiwa kufikisha asilimia ya makusanyo katika miradi ya maendeleo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment