Charles James, Miçhuzi TV
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amemshukuru Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini katika serikali yake na kumuahidi kuendelea kuitumikia nafasi hiyo akifuata maelekezo yake kwa weledi mkubwa.
Majaliwa amesema ni jambo la kumshukuru Rais kwa kumuamini katika nafasi hiyo ya uwaziri mkuu licha ya jana kufanya mabadiliko madogo kwenye baraza la mawaziri.
Waziri Mkuu Majaliwa ametumia nafasi hiyo kumpongeza Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Katanga akimsifu kwa namna ambavyo amekua akifanya kazi kwa uaminifu na mafanikio kwenye nafasi zote alizowahi kuzishika.
" Nimpongeze sana Balozi Katanga namfahamu vizuri sana amekua Katibu Mkuu wangu nikiwa Tamisemi, nimhakikishie ushirikiano, na kwa mawaziri wenzangu tunaahidi kwako Rais kuwa tupo tayari kuwatumikia watanzania.
Tukuahidi kwamba tutaendelea kukupa heshima na kutunza uaminifu wako kwetu tukifanya kazi kwa uweledi lengo likiwa kutekeleza ahadi za serikali yetu ya Chama cha Mapinduzi katika kuwatumikia wananchi kwa asilimia 100," Amesema Waziri Mkuu Majaliwa.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment