WEKUNDU WA MSIMBAZI WAWASILI BUKOBA | Tarimo Blog










Na Abdullatif Yunus, Michuzi TV.

KLABU ya Simba tayari imewasili Mkoani Kagera mapema Aprili 20, kusaka Alama Tatu dhidi ya wenyeji wao Wakata miwa wa Kagera Sukari, ambapo Timu hiyo imewasili ikiwa na Kikosi chake kamili.

Wakiongea katika Mkutano na waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Coffee Tree Hotel Walimu wa Timu zote Mbili wameonesha morali ya kupata ushindi kwa Timu zao,  huku kila mmoja akionesha kuheshimu mwenzake kimchezo.

Akizungumza kwa Upande wake Kocha wa Kikosi Cha Wakata miwa wa Kagera Francis Baraza amesema Timu yake ipo sawa licha ya kuwa na majeruhi wachache huku akimwaga sifa kwa wapinzani wao kwa kile alichokisema kuwa Simba ni miongoni mwa Timu kubwa Afrika hivyo atapambana kupata ushindi.

Naye nahodha wa Timu ya Wekundu wa Msimbazi Mohammed Hussein amekiri kuwa Timu yao imekuwa Ikipata wakati mgumu hasa wanapokutana na Kagera Sugar katika Uwanja wa Nyumbani, Hali ambayo husababisha kupata Matokeo kwa tabu Sana.

Timu ya Simba itafanya mazoezi Jioni hii katika Uwanja wa Kaitaba tayari kwa kujiandaa na Mchezo wao wa Jumatano hii.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2