KAZI yoyote, iwe ni ajira rasmi au kujihusisha na shughuli za uzalishaji kama vile kilimo na ujasiriamali ni msingi muhimu wa maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kimazingira ya jamii au nchi yoyote.
Kazi inawapa watu uhuru wa kiuchumi, fursa ya wa kushiriki katika maamuzi ya kijamii, na kuwaepusha wanajamii na vitendo vya uhalifu.
Tangu kuwasili kwake nchini mwaka 2017, mfumo unaoongoza wa kuagiza usafiri barani Afrika, Bolt imewawezesha maelfu wa madereva, waendeshaji wa vyombo vya moto na wale wanaotafuta ajira kupata fursa mpya za kujipatia na kujiongozea kipato.
Bolt ni mfumo wa kimtandao wa haraka, uhakika na nafuu zaidi wa kusafiri. Mfumo huu unamwezesha msafiri kuomba dereva amfuate moja kwa moja sehemu alipo na kumfikisha sehemu anapotaka kwenda, kwa matumizi ya mtandao.
“Madereva wanatumia mfumo wa Bolt kuanzisha biashara zao wenyewe na kupata mapato ya uhakika yanayowawezesha kuhudumia familia zao,” Remmy Eseka, Meneja wa Bolt nchini Tanzania anasema.
“Badhi ya madereva wanatumia magari na pikipiki zao wenyewe, na wengine wameajiriwa na wamiliki wa vyombo vya moto walioanzisha biashara zao za usafiri,” anaongeza.
Tathmini za Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS – 2018) kuhusu hali ya ajira nchini inaonesha kuwa asilimia 29% ya watanzania wameajiriwa katika sekta ya utoaji huduma – ambayo inajumuisha huduma za usafiri.
Ripoti Kuhusu Soko la Ajira Tanzania (2018) zinaonesha kuwa takriban asilimia 9.8% ya watu wote wazima hawakuwa na ajira katika kipindi hicho.
“Viwango vya ukosefu wa ajira ni kipimo muhimu cha matumizi ya nguvu kazi iliyopo. Ni vinaashiria uwezo wa uchumi kutoa fursa za kazi na ajira kwa wale ambao wana nia ya kufanya kazi lakini pamoja na kuwa wapo tayari na wanatafuta fursa hizo za kazi,b hawazipati” ripoti hiyo inabainisha.
Ripoti nyingine ya NBS “2019 - Takwimu za Tanzania” ya Juni 2020 inaonesha kuwa viwango vya ukosefu wa ajira vilishuka kutoka 10.1% mwaka 2015 hadi 9.6% mwaka 2019. Ripoti hiyo pia inasema kuwa idadi ya waajiriwa ilipanda kutoka 20.5 milioni hadi 22.5 milioni.
Pamoja na kuwa ni muhimu kwa nchi yoyote ile kuhakikisha upatikanaji wa fursa za kazi na ajira kwa watu wote wenye uwezo wa kufanya kazi, idadi kubwa ya watu, sio tu Tanzania bali duniani kote hawana kazi maalum – hivyo wanakoza fursa ya kushiriki katika uchumi wa nchi husika.
Huku idadi kubwa ya vijana ikizidi kungia katika soko finyu la ajira, ni muhimu kwa wadau wote kutafuta mbinu mpya za kuwawezesha kujipatia kipato.
Nchini, idadi kubwa ya watu, hasa vijana wamepata ahueni ya kipato kwa kujihusisha na huduma ya usafiri – iwe katika mabasi ya abiria, taxi au waendesha piki piki (boda boda) na piki piki za magurudumu matatu (bajaji).
Happiness Njunwa, ni dada anayefanya kazi ya kuendesha bajaji jijini Dar es Salaam. Anasema amefanya kazi hiyo kwa mkataba maalum na mwneye chombo kwa kipindi cha mwaka mmoja sasa, baada ya kukosa ajira za ofisini.
“Mfumo wa kuangiza usafiri kwa njia ya mtandao umetuongezea uhakika wa kupata abiria na kipato. Mfumo huu unatusaidia sana kwa maana unatuunganisha moja kwa moja na watu wanaohitaji usafiri, wakati na mahali ambapo usafiri unahitajika. Umetupunguzia gharama za kuzunguka ovyo au kukaa kijiweni tukisubiri abiria. Sasa kupitia mtandao mteja anaweza kujua usafiri upo wapi na dereva nawe ukajua mteja yupo wapi na anahitaji kwenda wapi,” anabainisha.
Nchini Tanzania, inakadiriwa kuwa zaidi ya wanafunzi 800,000 wanafuzu kutoka vyuo vya elimu ya juu na vya ufundi kila mwaka. Kwa hiyo ukuaji wa teknologia ya kugawana rasilimali kami le inayotumia na mfumo wa kuagiza usafiri kwa njia ya mtandao ni suluhisho sahihi la ukosefu wa ajira kwa vijana.
“Mfumo wao pia ni maalum kwa usalama wa dereva na mteja. Dereva au abiria anaweza kutoa taarifa ya tatizo lolote linalojitokeza haraka kwa njia ya mtandao na kupata msaada haraka katika eneo husika. Hii imetuwezesha madereva wa kike kuwa na uhakika zaidi wa kufanya kazi, hata nyakati za usiku,” alisema Happiness.
“Tunafurahi kutoa fursa za kazi na za biashara zinazowawezesha watu kujipatia kipato na kuboresha maishayao. Pia tunafurahia kuwezesha watanzania wanaoishi Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Dodoma kupata usafiri wa uhakika kwa bei nafuu,” Mkurugenzi wa Bolt anaongeza.
Huku dunia ikikumbuka mchango mkubwa wa maendeleo ulioletwa na wafanyakazi, teknologia mpya kama ile ya Bolt sasa inafungua ukurasa mpya unaobadilisha maana ya kazi, ajira na biashara. Ni njia mpya yenye uwezo mkubwa wa kuwezesha kizazi kijacho kujipatia kipato na kuwa sehemu ya maendeleo ya nchi.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment