Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv
KIKUNDI cha Maendeleo ya Jamii kinachoendesha Ukumbi wa Starehe Bar ya Pittop and Grill Mbezi Beach kimetoa msaada wa viti vya walimu pamoja na kutandika mabomba kwenye vyoo vitatu katika Shule ya Msingi Jangwani iliyopo Manispaa ya Kinondoni Mkoani Dar es Salaam.
Akizungumza baada ya kukabidhi msaada huo Mwenyekiti wa Kikundi hicho Paul Kivumbi amesema kuwa hawana budi kuchangia shule hiyo kwani iko Karibu eneo la biashara yao.
Kivumbi amesema kuwa baada ya kufanya utafiti wa kuweza kusaidia walikutana na uongozi wa Mtaa na kukubaliana wasaidie katika Shule hiyo.
Kivumbi amesema kuwa wanaangalia baadae wasaidie bati katika Shule hiyo kwani zinaonyesha uchakavu ambao kama wao hawakubaliani kuona shule hiyo ikiwa katika mazingira yasiyoridhisha.
"Sisi kama jamii tunayoizunguka shule ni wajibu wetu kusaidia kwani ni watoto wetu wanasoma ambao wanahitaji kusoma mazingira yaliyo bora na hakuna kila kitu tuiachie Serikali"amesema Kivumbi.
Aidha amesema kuwa watu wengine waguswe na shule hiyo kwa kusaidia maeneo mbalimbali kwani changamoto katika shule hazikosekani.
Nae Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Jangwani Christina Luoga amesema kuwa kikundi hicho kimefanya jambo zuri kwa kutandika mabomba kwenda vyooni.
Amesema wanafunzi wamekuwa wakichota Maji na kupeleka hiyo ni changamoto kwa wasichana wakati wakiwa katika kipindi cha hedhi.
Amesema kuwa wameona mbali sana Kama uongozi wa shule unashukuru kwa kuonyesha wanajali walimu pamoja na wanafunzi.
Mkuu wa Shule hiyo ametoa wito watu wengine wanaweza kuendelea kusaidia sehemu ambazo zinatakiwa kuboreshwa huku Serikali ikiwa katika mikakati ya uboreshaji wa shule .
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment