KISA BAJAJI, DALADALA ZAGOMA NJOMBE | Tarimo Blog


Na Amiri Kilagalila, Njombe

MADEREVA wa usafirishaji abiria kwa njia ya magari madogo (daladala) mjini Njombe,wameamua kusitisha usafirishaji kwa muda usiojulikana kwa madai ya kushinikiza wasafirishaji abiria kwa njia ya bajaji kufuata utaratibu na sheria za usafirishaji.

Wakizungumza na vyombo vya habari wasafirishaji hao akiwemo Frank Kinzumbe na  Nickolaus Kihovele wamaesema sababu ya mgomo huo ni kupigania sheria na haki ili zifuatwe kwa mujibu wa chombo husika na kuepusha migongano ya kibiashara barabarani.

Aidha wameiomba serikali kupitia vyombo husika kushughulikia malalamiko yao kwa kuwa wamekwisha fikisha malalamiko dhidi ya wasafirishaji wa kutumia bajaji kuharibu utaratibu wa usafirishaji na kuwasababishia hasara kutokana na kukosa abiria.

“Tunachopigania sisi ni sheria zifuatwe,kwasababu tulikuabaliana kila watu wafanye kazi kwa mujibu wa utaratibu na ukiangalia Dalala haiwezi kwenda Kibena na watu wanne kwasababu barabarani wateja wamechukuliwa na bajaji zinazofanya kazi kama daladala”alisema Frank Kinzumbe

Nickolaus Kihovele amesema “Huu mgomo utadumu mpaka pale suluhisho litakapopatikana kwasababu tangu wiki iliyopita walisema wanalifanyia kazi lakini tunaona bado bajaji tunapishana nazo kweny njia zetu na zinazidi kuongezeka siku hadi siku”

Joyce Nungwa ni afisa mfawidhi wa mamlaka ya usafirishaji ardhini LATRA mkoa wa Njombe, amesema tatizo la muingiliano wa vyombo hivyo umekuwa ukijitokeza mara kwa mara na wameendelea kushughulikia huku wakikili kupokea malalamiko ya hivi karibuni kutoka kwa wasafirishaji hao lakini wakati wakiendelea na mchakato kumaliza tatizo hilo wanashangaa kuona mgomo huo umetokea.

“Tulishakubaliana na bajaji kuhakikisha wanafanya kazi kama leseni inavyosema kwa kukodishalakini hata hivyo toka siku ya jumatano tulikuwa kwenye utekelezaji mpaka leo napata taarifa za kuwa kuna mgomo”alisema Joyce Nungwa

Naye Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah amesema jeshi hilo halipendi kuona watu wana fanya kazi kwa migongano hiyo wako tayari kushughulika na mgogoro huo huku akiwaomba Madereva kurejesha vyombo hivyo barabarani.

“Hili swala migongano usalama unakuwa haupo na tunaomba watu wasifanye kwa migongano kwasababu haileti maendeleo naamini hili swala tutalishughulikia”alisema Kamanda Issah

Hata hivyo amesema ili kuondoa adha wanayokumbana nayo abiria na watumiaji wa vyombo hivyo wameomba vyombo vingine vyenye njia za karibu kusaidia kubeba abiria wanaohitaji kufika maeneo mbali mbali kwa ajili ya shughuli zao huku wakiendelea kushughulika na mgogoro huo.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2