KIWANDA CHA DANGOTE MKOANI MTWARA KIKO MBIONI KUBADILISHA TAKA ZA PLASTIKI KUWA BIDHAA | Tarimo Blog

 Na Mwaandishi Wetu Mtwara

KIWANDA cha Dangote Mkoani Mtwara kiko mbioni kuanza kubadilisha taka za plastiki kuwa bidhaa mpya ili kusaidia katika kusafisha na kuokoa mazingira ya kiwanda na ya wananchi wanaowazunguka.

Meneja Mkuu wa Uzalishaji katika kiwanda  hicho Abayomi Awofudu  amesema haya wakati akikabidhi msaada wa mapipa ya kukusanyia taka ngumu yaliyotolewa na kiwanda hicho kwa uongozi wa Kijiji cha Hiari katika halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.

Kiwanda hicho cha Dangote ambacho  kipo katika maeneo ya Kijiji cha Hiari kitakuwa na utaratibu wa kubadilisha taka hizo ngumu haswa plastiki na kutengeneza bidhaa mpya zitakazotumika tena.

“Nina furaha sana leo kukabidhi mapipa haya kwa uongozi wa kijiji ili waweze kukusanya taka na kuzihifadhi sehem sahihi ili kulinda mazingira yetu na uchafu,” amesema.

Awofudu amesema mapipa hayo yatatumika katika kukusanya taka mbalimbali kwa kuzitenganisha huku mapipa mengine yakitumika kwa kukusanya taka za plastiki tu ambazo baadae zitapelekwa katika kiwanda cha Dangote na kubadilishwa kuwa bidhaa mpya.

Amesema wakati anakuja kufanya kazi kwenye kiwanda cha Dangote Mkoani hapa alikuta taka nyingi zinazagaa kwenye maeneo ya kiwanda kitu ambacho amesema ni hatari kwa afya ya binadam na hata kwa kiwanda chenyewe.

“Mazingira yakiwa masafi watu wanakuwa pia na afya nzuri na kuendelea kufanya kazi,”amesema na kuongeza kuwa ameshaagiza uongozi wa mazingira katika kiwanda cha dangote kusimimia zoezi hilo la kukusanya na kubadilisha taka za plastiki kuwa bidhaa mpya.

Kaimu Mkurungezi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara John Nkoko ameushuruku uongozi wa Dangote kwa kutoa mapima hayo ambayo yatasaidia kijiji katika kukusanya taka kutoka maeneo mbalimbali ya kijiji cha Hiari.

“Kwa niaba ya Halmashauri, sisi tumefarijika kwa kiwanda kukubali na kuridhia kutoa mapipa haya kwa ajili ya kukusanyia taka kabla ya kuzipeleka kwenye eneo la dampo,” amesema.

Amesema umekuwa ni mda mwafaja na wakati mzuri ambapo pia Halmshauri itakuwa inaungana na wengine katika kuadhimisha siku ya mazingira duniani. Siku ya maizngira huadhimishwa kuanzia tarehe moja mpka tarehe tano mwezi Juni.

Amewaomba wananchi na uongozi wa kijiji kuhakikisha kuwa mapipa hayo yanatumika vizuri ipasavyo ili kuhifadhi taka kwa kuzitenganisha ili zile ambazo zinawea kubadilishwa kuwa bidhaa mpya zipatikane kwa uarahisi na kupelekwa sehem sahihi.

Amesema sheria ndogo zitatumika kikamilifu kuhakikisha zoezi hilo la kukusanya taka linatekelezwa kikamilifu huku akitoa onyo kwa wale watakaokiuka taratibu na kutupa taka hovyo kuchukuliwa hatua.


 
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2